Mfalme MOHAMMED VI wa MOROCCO aanza ziara yake nchini
Mfalme
MOHAMMED wa SITA wa MOROCCO amewasili nchini kwa ziara ya kiserikali
yenye lengo la kuimarisha uhusiano baina ya MOROCCO na TANZANIA
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli
akimlaki Mfalme wa Morocco Mohammed VI mara baada ya kuwasili katika
Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere
Mara baada ya ya kuwasili katika uwanja wa Ndege wa
kimataifa wa JULIUS NYERERE jijini DSM Mfalme MOHAMED wa SITA
alipokelewa na mwenyeji wake Rais DKT JOHN MAGUFULI ukaimbwa wimbo wa
taifa na kupigiwa mizinga 21 .Katika ziara yake hapa nchini mfalme huyo pamoja na mambo mengine, atasaini mikataba 11 ya ushirikiano katika sekta za kilimo, gesi mafuta reli ya LIGANGA na MCHUCHUMA na sekta ya utalii.
Pia atatembelea ZANZIBAR na kukutana na Rais ALI MOHAMED SHEIN na pia atatembelea Mamlaka ya Hifadhi ya NGORONGORO na kujionea vivutio vilivyopo nchini.
No comments