Benki Kuu (BoT) yatolea ufafanuzi taarifa za kutotumika tena noti ya shilingi 500
Benki Kuu ya
inapenda kuwafahamisha wananchi wote kuwa habari inayoenea katika
mitandao mbalimbali ya kijamii kwamba noti ya shilingi mia tano
haitatumika tena baada ya Disemba 31, 2016 sio taarifa ya kweli na ni
uvumi unaopaswa kupuuzwa.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi wa Huduma za kibenki BoT, Marcian Kobello
ambapo alifafanua kuwa noti ya shilingi 500 itaendelea kuwepo katika
mzunguko sambamba na ile sarafu ya shilingi 500 hadi pale noti hiyo
itakapotoweka mikononi mwa wananchi.
Aidha, Kobello amewataka wananchi kupuuza taarifa zinazoeleza vinginevyo kwani si za kweli.
Serikali
iliamua kuleta sarafu ya TZS 500 baada ya kuwepo malalamiko kuwa noti
ya TZS 500 ambayo ndiyo inazunguka zaidi inachakaa mapema sana.
No comments