• Breaking News

    Wimbi la mauaji ya viongozi lazua taharuki PWANI


    Wakazi wa wilaya za mkuranga na Kibiti mkoani PWANI wamekumbwa na taharuki kufuatia kuibuka kwa wimbi la mauaji
    Kamanda wa polisi mkoa wa PWANI BONAVENTURA MUSHONGI
     
    Wakazi wa wilaya  za mkuranga na Kibiti mkoani PWANI wamekumbwa na taharuki kufuatia kuibuka kwa wimbi la mauaji ya wenye viti na watendaji wa serikali za vijiji  wanaouwawa kwa kuvamiwa na kupigwa risasi na watu wasiojulikana.
    Kamanda wa polisi mkoa wa PWANI BONAVENTURA MUSHONGI amekiri kuibuka kwa mauaji hayo ambayo yameonekana kuwalenga watendaji wa vijiji ambapo wauaji huwavamia watendaji hao nyumbani au wakiwa ofisini kwa kutumia pikipiki na kisha kuwapiga risasi na kuondoka.
    Kamanda polisi mkoa wa PWANI BONIVENTURA  MUSHONGI amewaambia waandishi wa habari kuwa tangu kuanza kwa mauaji hayo watu watatu wameuwawa wakiwemo wenyeviti wawili wa vijiji waliouwawa  wilaya ya Mkuranga ambapo mwenyekiti wa kijiji cha KIMANZICHANA alipigwa risasi wiki mbili zilizopita majira ya saa tano mchana akiwa ofisini kwake na tukio jingine limetokea usiku wa kuamkia jana ambapo afisa mtendaji wa kijiji Nyambunda kilichopo wilaya mpya ya KIBITI ameuwawa kwa kupigwa risasi na watu watatu waliofika nyumbani kwake majira ya saa mbili usiku wakiwa wamepakiwa kwenye pikipiki aina ya BOXER.
    Kufuatia hali hiyo jeshi la polisi linafanya msako mkali kutafuta wahusika wa mauaji hayo na  kuwaomba wananchi kutoa ushirikianao pindi wanapomtilia mtu yeyote mashaka kwamba anahusika na mauaji hayo kwa namna moja au nyingine.

    No comments

    Post Top Ad