Mtendaji akamatwa kwa kuhujumu zaidi ya shilingi milioni 95
Mtendaji
wa Kata ya GILAY LUMBWA iliyopo katika wilaya ya LONGIDO mkoani ARUSHA,
PAULO LUCAS anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma za kuhujumu
fedha
Mkuu wa Mkoa wa ARUSHA, MRISHO GAMBO
Mtendaji wa Kata ya GILAY LUMBWA iliyopo katika wilaya
ya LONGIDO mkoani ARUSHA, PAULO LUCAS anashikiliwa na jeshi la polisi
kwa tuhuma za kuhujumu fedha zaidi ya Milioni 95 zilizochangwa
na wananchi kwa ajili ya ujenzi wa shule ya sekondari ya
FILAMINGO ikiwa ni pamoja na vyumba vya madarasa, maabara na mabweni ya
wanafunzi.Hatua hiyo imefikiwa baada ya taarifa iliyosomwa na mkuu wa shule hiyo kuonyesha kiasi kidogo cha fedha ikilinganishwa na fedha zilichochangwa na wananchi huku Wananchi nao wakidai wamechanga mifugo na fedha taslimu hivyo taarifa hiyo siyo sahihi jambo ambalo Mkuu wa Mkoa wa ARUSHA, MRISHO GAMBO alitaka kupewa taarifa na Mkaguzi wa ndani wa Halimashauri hiyo ndipo ubadhilifu ukabainika.
Mkurugenzi wa Halimashauri hiyo JUMA MHINA,amesema amepokea taarifa ya Mkaguzi wa ndani inayo onyesha ubadhilifu wafedha katika ujenzi wa shule hivyo Mtendaji huyo hanabudi kuwa mikononi mwa Polisi akisubiri kufunguliwa mashitaka kwa kosa hilo
No comments