KINONDONI yapata meya mpya
Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya KINONDONI jijini DAR ES SALAAM, wamemchagua BENJAMIN SITTA kutoka chama cha mapinduzi CCM Kuwa meya mpya wa manisipaa ya KINONDONI baada ya kupata kura kumi na nane.
Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika katika manisipaa ya Kinondoni, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo AARON KAGOROMJULI amesema SITTA amepata ushindi huo kwa kupigiwa kura zote kumi na nane ambapo wajumbe 16 kutoka vyama vya upinzani ambavyo ni Chadema, na CUF walisusia kushiriki katika uchaguzi huo.
Uchaguzi wa meya Halmashauri ya wilaya ya KINONDONI umekumbwa na changamoto mbalimbali, ikiwemo utata wa makazi ya mmoja wa wajumbe wake Profesa JOYCE NDALICHAKO utata ambao umetolewa ufafanuzi, kwa utambulisho wa makazi kabla ya kuapishwa kwa Profesa NDALICHAKO.
Uchaguzi huo wa meya umefanyika baada ya wilaya ya KINONDONI kugawanywa, na hivyo kuzaa wilaya mpya ya UBUNGO
No comments