• Breaking News

    TPDC kujenga kiwanda Lindi


    Shirika la Maendeleo ya Petroli Nchini -TPDC kwa kushirikiana na kampuni za kimataifa za mafuta inatarajia kujenga kiwanda cha kuchakata gesi asilia LNG katika eneo la Likong’o katika Manispaa ya Lindi
    Akifungua  mkutano  wa wadau wa gesi na kampuni za utafiti wa gesi  jijini Dar Es Salaam Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nishati na Madini Profesa James Mdoe amesema kiwanda hicho kitaifanya gesi kuwa kimiminika na kuwekwa katika mitungi kwa ajili ya matumizi ya majumbani na viwandani.

    Naye Mkurugenzi wa utafiti wa gesi mkondo wa chini wa TPDC, Kelvin Komba amesema kazi ya ujenzi wa kiwanda hicho utaanza baada ya taratibu za kimikataba kukamilika.

    Egidius Audax

    No comments

    Post Top Ad