• Breaking News

    Swissport kujenga bohari


    Kampuni ya upakuaji na upakiaji mizigo kwenye ndege ya Swissport Tanzania imewekeza shilingi bilioni 26 kujenga bohari ya kisasa ya mizigo katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere jijini Dar Es Salaam
    Swissport kujenga bohari
    Akizungumza wakati wa uzinduzi wa  jengo hilo, Afisa Mtendaji Mkuu wa kampuni hiyo Gaudence Temu amesema bohari hiyo ina mitambo ya baridi ya kuhifadhi mizigo inayoharibika haraka, mitambo ya ukaguzi, mizani, vyumba vya kuhifadhia wanyama wadogo na mizigo ya kawaida.

    Katika hatua nyingine Mkurugenzi wa Fedha wa kampuni hiyo Mrisho Yasini amesema Swissport imepata tuzo ya kimataifa inayotambuliwa na Shirikisho la Usafiri wa Kimataifa wa Anga ya ISAGO kwa kutambua huduma bora inazozitoa kwa abiria wa ndege na mizigo yao.

    Stanley Ganzel

    No comments

    Post Top Ad