Serikali yasema mipaka ya nchi ni salama
Serikali
imewahakikishia watanzania kuwa mipaka yote ya nchi iko salama na
katika baadhi ya maeneo ambapo kulitokea migongano mazungumzo
yanaendelea vizuri
Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa leo 10 Mei,
2016, Bungeni mjini Dodoma
Serikali imewahakikishia watanzania kuwa mipaka yote ya nchi
iko salama na katika baadhi ya maeneo ambapo kulitokea migongano
mazungumzo yanaendelea vizuri yakiongozwa na Wizara ya Mambo ya Nje,
Afrika, Mashariki, Kikanda na Kimataifa.Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenza Taifa Dkt. Hussein Mwinyi wakati akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2016/2017.
Amesema serikali inaendelea kuboresha Jeshi liwe la kisasa zaidi.
Waziri Mwinyi amesema maagizo yote yaliyotolewa na Rais John Magufuli alipozindua bunge la 11 yameingizwa kwenye mpango wa utekelezaji wa wizara yake na kwamba wanaendelea kuwa macho kila pande ya mipaka kutokana na uwepo wa vikundi mbalimbali vya kigaidi kama Al Shabab, Al qaida, Boko Haram na Islamic State.
Kwa upande wao Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje Ulinzi na Usalama Adadi Rajabu na Msemaji wa kambi rasmi ya upinzani bungeni katika wizara hiyo Juma Hamad Omar wameitaka serikali kuhakikisha fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya wizara hiyo zinatolewa kwa wakati ili jeshi litekeleze malengo na majukumu yake ipasavyo.
Elisha Elia
No comments