• Breaking News

    Polisi waua mtu anayesadikiwa kuwa jambazi Kagera


    Vitendo vya utekaji na uporaji wa mashine za mitumbwi na mali nyingine katika baadhi ya visiwa vilivyopo ndani ya ziwa Victoria mkoani Kagera
    Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kagera Augustino Ollomi
    Vitendo vya utekaji na uporaji wa mashine za mitumbwi na mali nyingine katika baadhi ya visiwa vilivyopo ndani ya ziwa Victoria mkoani Kagera vimeendelea na hivyo kusababisha hali ya wasiwasi kwa wakazi wa visiwa hivyo.

    Katika tukio la hivi karibuni mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni jambazi ameuawa wakati wa mapambano ya kurushiana risasi baina ya Polisi na majambazi waliovamia kisiwa cha Mazinga wilayani Muleba na kupora mashine na mtumbwi uliokuwa na samaki.

    Kamanda wa Polisi wa mkoa wa Kagera Augustino Ollomi amesema katika mapambano hayo ya kurushiana risasi yaliyoendelea hadi katika kisiwa cha Ghana karibu na wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, mtu mmoja anayesadikiwa kuwa jambazi aliuawa huku mwenzake mmoja akijisalimisha.

    Kamanda huyo wa Polisi wa mkoa wa Kagera amehimiza dhana ya ulinzi shirikishi katika visiwa hivyo.

    Charles Mwebeya

    No comments

    Post Top Ad