Rais Mstaafu Kikwete atembelea daraja la Nyerere
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Rais mstaafu Jakaya Kikwete ametembelea daraja la Nyerere lililoko jijini Dar Es Salaam
Kando ya ziara hiyo Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Joseph Nyamhanga ametangaza rasmi tozo kwa vyombo vya usafiri vitakavyopita kwenye daraja la Nyerere lililopo jijini Dar Es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya ziara ya Rais Mstaafu wa awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete iliyokua na lengo la kuangalia daraja hilo, Nyamhanga amesema tozo hizo zitatofautiana kulingana na ukubwa wa chombo husika.
Mkurugenzi wa uwekezaji kutoka NSSF, Yacoub Kidula amesema tozo hizo zitaanza kutumika rasmi tarehe 14 mwezi huu.
Norah Uledi
No comments