• Breaking News

    Wananchi wa ARMENIA wafanya kumbukumbu ya mauaji ya halaiki


    Mamia ya wananchi wa ARMENIA, wamejitokeza katika mitaa ya mji mkuu wan chi hiyo, kukumbuka mauji ya raia wenzao waliouawa katika mauaji ya halaiki
    Wananchi wa ARMENIA wafanya kumbukumbu ya mauaji ya halaiki
    Mamia ya wananchi wa ARMENIA, wamejitokeza katika mitaa ya mji mkuu wa nchi hiyo, kukumbuka mauji ya raia wenzao waliouawa katika mauaji ya halaiki wakati wa utawala wa OTTOMAN, kwenye karne ya KUMI na tano.


    Watu hao walijitokeza na kuwasha mienge ya matumani mapya huku wakichoma bendera za nchi za UTURUKI na AZABAIJAN, nchi ambazo kwa wakati huo zilishiriki katika mauaji ya watu wa jamii ya ARMENIA.

    Utawala wa kifalme wa OTTOMAN, wakati huo, ulikuwa ni kutoka nchini UTURUKI na ulimiliki sehemu kubwa ya dunia.

    Watu hao wanasema, wameandamana wakitaka serikali ya UTURUKI, kutambua kuwa mauji yaliyofanywa na nchi hiyo wakati wa utawala wa OTTOMAN, yalikuwa ni uhalifu dhidi ya ubinadamu, na wananchi wanataka nchi hiyo kuwaomba radhi.

    Wamesema, babu na bibi zao waliowapoteza katika kipindi hicho watawakumbuka daima, na wanataka jumuiya ya kimataifa ikumbuke kile kilichotokea katika jamii yao na kukilaani ili kisitokee tena.

    April 25, 2016
    JUDICA LOSAI

    No comments

    Post Top Ad