• Breaking News

    Kiwanda cha sukari Kilombero chasaidia jamii


    Kiwanda cha sukari cha Kilombero kimetumia zaidi ya shilingi milioni 200 katika ujenzi wa miradi mbalimbali ya kijamii katika nyanja za afya na elimu katika wilaya za Kilombero na Kilosa mkoani Morogoro
    Akikabidhi bweni la wasichana la shule ya sekondari ya Ruhembe lililojengwa kwa gharama ya shilingi milioni 90, Meneja wa Mfuko wa kusaidia Jamii wa kiwanda hicho Mary Elizabeth ameitaja miradi mingine kuwa ni ujenzi wa madarasa katika shule za msingi za Ilunga na Muungano.

    Naye Mkuu wa shule hiyo Johannes Ruekulam amesema bweni hilo lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 48 litaondoa usumbufu wa kutembea kwa zaidi ya kilomita 40 kila siku kwa wasichana wa shule yake.

    Na Fatma Matulanga
    25 April 2016

    No comments

    Post Top Ad