Ndege inayotumia mwanga yatua salama CALIFORNIA
Hatimaye
ndege inayotumia mwanga wa jua kijiendesha imewasili katika uwanja wa
ndege wa CALIFORNIA nchini MAREKANI, baada kukatiza bila matatizo bahari
kuu ya ATLANTIKI
Ndege hiyo imewasili nchini MAREKANI, baada ya kuruka kutoka
katika visiwa vya HAWAII, siku ya Alhamisi wiki iliyopita, ikiwa ni
awamu wa TISA ya majaribio yake wa safari za anga.
Ndege hiyo inatumia mwanga wa jua kujiendesha katika shughuli zake zote na hivyo kuweka historia ya dunia, kuwa ndege ya kwanza kuruka angani ikitumia nishati ya mwanga wa jua badala ya kutumia mafuta.
Kwa mara ya kwanza ndege hiyo ilianza majaribio yake ya safari za anga mwezi Machi mwaka jana katika uwanja wa ndege wa ABUDABI.
Licha ya kupata hitilafu ikiwa angani na kulazimisha kusitisha safari zake za muda baada ya kuanza safari yake rasmi nchini JAPAN, ndege hiyo ndiyo imekuwa ndege ya kwanza kufanya safari zake kwa siku tano mfululizo ikitumia mwanga wa jua.
Lubani wa ndege hiyo ya SOLA anasema, sasa ni wakati mufaka kwa serikali mbalimbali duniani, kupitisha sheria mpya za matumizi ya ndege hiyo, ambayo ni rafiki wa mazingira na kuachana na ndege zinazochafua mazingira, ambazo hutumia mafuta.
April 25, 2016
JUDICA LOSAI

No comments