• Breaking News

    Israel yamwachia huru binti wa kiPalestina


    Serikali ya ISRAEL imemwanchia huru binti mwenye miaka KUMI NA MIWILI, kutoka katika Mamlaka ya PALESTINA, aliyekuwa akishikiliwa katika magereza ya nchi hiyo

    Serikali ya ISRAEL imemwanchia huru binti mwenye miaka KUMI NA MIWILI, kutoka katika Mamlaka ya PALESTINA, aliyekuwa akishikiliwa katika magereza ya nchi hiyo, na kuwa mfungwa mdogo kuliko wote kuachiwa nchini humo.


    Binti huyo ameachiwa huru, baada ya malalamiko mengi kutoka kwa wanaharaka na watu wanaotetea haki za binadamu duniani kuhusiana na umri wake.

    Binti huyo kutoka katika Mamlaka ya PALESTINA alikamatwa kwa tuhuma za kukutwa na kisu, katika makazi ya wayahudi huko kwenye Ukingo wa Magharibi wa mto JORDAN, karibu na nyumbani kwao.

    Vikundi vya kutetea haki za binadamu vinasema zaidi ya watoto 125 kutoka katika Mamlaka hayo, bado wanashikiliwa kwenye magereza nchini ISRAEL.

    April 25, 2016
    JUDICA LOSAI

    No comments

    Post Top Ad