Rais ZUMA afanya ziara nchini IRAN
Rais JACOB ZUMA wa Afrika Kusini yuko nchini Iran kwa ziara ya siku mbili
Rais ZUMA ameongozana na ujumbe wa maafisa wa serikali na
wafanyabiashara anatarajiwa kufanya mazungumzo kuhusu kujenga tena
uhusiano wa kibiashara, ambao ulizuiliwa wakati IRAN ilipowekewa vikwazo
vya kimataifa, kwa sababu ya mradi wake wa nyuklia.
Rais ZUMA amesema baada ya vikwazo hivyo kuondolewa zimefunguka fursa mpya za kufanya biashara baina ya IRAN na bara la Afrika.
Bidhaa ambazo Afrika Kusini iliiuzia IRAN mwaka 2014 zilikuwa ni asilimia 20 ya kiwango cha miaka sita iliyopita.
April 25, 2016
Aaron Mrikaria

No comments