• Breaking News

    Bandari ya TANGA yashinda zabuni ya kujenga bomba la mafuta


    Waziri wa Nishati na Madini Profesa SOSPETER MUHONGO amesema bandari ya TANGA imeshinda zabuni ya ujenzi wa bomba la mafuta Kutoka Ziwa ALBERT nchini Uganda
    Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, akonyesha kwa wanahabari, mpango wa ujenzi wa Bomba la Mafuta kutoka nchini Uganda mpaka jijini Tanga
    Waziri wa Nishati na Madini Profesa SOSPETER MUHONGO amesema bandari ya TANGA imeshinda zabuni ya ujenzi wa bomba la mafuta Kutoka Ziwa ALBERT nchini Uganda hadi  bandari ya TANGA kutokana na kigezo cha kuwa na kina kirefu na mazingira ya kijiografia ambayo yanaiwezesha kustahimili mawimbi makali ya bahari.


    Akizungumzia ushindi huo ametaja sababu nyingine ya Tanzania kuchaguliwa katika mradi huo wa bomba la mafuta kuwa ni njia ambayo bomba hilo litapita ni ya mteremko hali itakayosaidia kupunguza gharama za kupampu mafuta.

    Aidha sababu zingine ni usalama wa Tanzania ukilinganisha na nchi kama KENYA iliyokumbwa na matukio ya ugaidi pamoja na  uzoefu mkubwa katika uendeshaji wa mabomba ya mafuta kama lile la TAZAMA.

    MUHONGO ameainisha baadhi ya faida ambazo Tanzania itazipata ni ajira kwa vijana.


    April 25, 2016
    DOMINIC MOKIWA

    No comments

    Post Top Ad