• Breaking News

    AZAM yatinga fainali



    Timu ya AZAM imetinga fainali ya michuano ya kombe la shirikisho baada ya kuifunga timu ya MWADUI FC kwa mikwaju ya penati MITANO kwa minne katika mchezo uliofanyika uwanja wa KAMBARAGE huku SHINYANGA

    Katika mchezo huo timu hizo zilifungana magoli mawili kwa mawili baada ya dakika 120 za mchezo na kuamuliwa kwa mikwaji ya penati na AZAM kuibuka na ushindi wa penati tano kwa nne.

    Katika nusu fainali nyingine iliyofanyika huko mkoani TANGA mchezo kati ya YANGA na COASTAL UNION ya TANGA umeshindwa kumalizika baada ya kutokea kwa vurugu .

    Kabla ya kuanza kwa VURUGU hizo yanga ilikuwa inaongoza kwa magoli MAWILI kwa MOJA hivyo majibu ya mchezo huo yatangazwa mara baada ya ripoti ya kamisaa.

    April 25, 2016
    EVANCE MHANDO

    No comments

    Post Top Ad