CCM Yatoa Onyo kwa makada wake Wanaolalamika Baada ya Kutumbuliwa na Rais
Chama
cha Mapinduzi (CCM) kimeibuka na kukemea vikali kauli zinazotolewa na
viongozi au makada wa chama hicho wambao wametenguliwa na Rais Dkt John
Pombe Magufuli katika nafasi zao mbalimbali walizokuwa wakishikilia.
Katibu
wa Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), Siasa na Uhusiano wa Kimataifa, Kanali
Mstaafu Ngemela Lubinga aliyasema hayo juzi akizungumza Mjini Iringa
katika mkutano na wanafunzi wa vyuo vikuu vilivyomo mkoani humo ambao ni
wananchama na pia viongozi wa chama hicho katika ngazi ya matawi na
kata.
Lubinga
aliwataka makada hao walioteuliwa na kisha kutemwa na Rais Dkt
Mwagufuli ambaye pia ni Mwenyeketi wa CCM Taifa, kuacha kulalamika na
kupiga kelele badala yake wakubiliane na mabadiliko hayo kwa nia ya
kuheshimu maamuzi ya Ikulu kwa uamuzi uliochukuliwa dhidi yao.
Licha
ya kuwa kiongozi huyo hakutaja majina ya viongozi aliowataka kuheshimu
maamuzi ya Ikulu, lakini ni dhahiri kuwa miongoni mwa waliolengwa ni
Mbunge wa Mtama (CCM), Nape Moses Nnauye ambaye alitenguliwa katika
nafasi yake aliyokuwa ya Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo
nafasi aliyoitumikia kwa kipindi cha miezi 15.
Nape
alitenguliwa katika nafasi hiyo ikiwa ni saa chache tu tangu alipopokea
ripoti ya kuvamiwa kwa kituo cha Clouds Media Group ambapo ripoti hiyo
ilithibitisha kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam ndiye aliyehusika
katika tukio hilo.
Nafasi
ya Nape ilichukuliwa na aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Dkt.
Harrison George Mwakyembe ambaye naye nafasi yake ikajazwa na Mbunge wa
kuteuliwa na Rais, Prof. Palamagamba Aidan John Kabudi ambaye ni mbobezi
katika taaluma ya sheria.
Mwingine
ambaye licha ya kuwa hakuenguliwa na Rais moja kwa moja lakini
alionyesha kutoridhishwa na mchakato wa kuenguliwa kwake ndani ya CCM ni
aliyekuwa Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki, Shyrose Bhanji. Yeye
alienguliwa alipotaka kugombea kwa mara ya pili, na tangu hapo amekuwa
akilalamika kwa madai kuwa njia zilizotumika hazikuwa za haki.
“Rais
anapoteua kiongozi na kumpa dhamana ni kwamba anaona kuwa unahitajika,
lakini inapofika mahali amekuondoa ujue mazingira yale huwezi kuyamudu
na anakuokoa ili usipate laana. Baadhi ya viongozi wameondolewa
madarakani, lakini wamebaki wakilalamika mitaani ovyo.” alisema Kanali Lubinga.
Lubinga
alisema kuwa chama hicho sasa kimejikita kuhakikisha kuwa kinarejesha
nidhamu na uwajibikaji ndani ya chama na serikali ili viongozi wote
waliochaguliwa na kuteuliwa wafanye kazi kwa maslahi mapana ya taifa na
wananchi.

No comments