SIMULIZI YA MAPENZI: FACEBOOK SEHEMU YA 04
sehemu ya 03
ILIPOISHIA....................
"Mh! amesema atatumia kama wiki mbili hivi,njoo basi unipe 'kampan' kiaina"
Yalikuwa mazungumzo kwa njia ya simu kati ya Adam na Reshmail yaliyokatishwa na na mlio wa 'low battery' katika simu ya Reshmail "Baby boy tutaongea kesho,pole sana na ninakupenda sana" alimaliza Resh na simu ikawa imezima.
"Eveline nataka kwenda Mwanza" asubuh ya siku iliyofuata Resh alimwambia Eve.
"He! makubwa haya,imekuwaje kwan shoga" aliduwaa.
"Mi sijui lakin nataka kwenda tu" alisema Reshmail "Haya lini wataka kwenda?"
"Hata kesho mi naenda tu" "Mh! sikuwez haya jiandae kutoroka coz ruhusa hapa kupata sahau" "Vyovyote poa ninachotaka ni kuondoka na kwenda Mwanza that's all" alijibu kijasiri Resh hali iliyomduwaza eveline.
USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA
INAENDELEA........
"Reshmail hayupo? mbona jana alikuwa hapa ofisin?"
mwalimu wa zamu alikuwa anamuuliza mwanafunzi aliyeagizwa kumuita Reshmail
baada ya mama yake kuwa amefika,"Hata mi sijui mwalimu"
"Hapana sio jambo la kawaida reshmail kutokuwa mazingira ya
shule tena jumatatu! hebu mwambie time-keeper agonge kengere mara moja"
aliamrisha mwalimu.
******
Hakuwa hata na chembe ya utani Reshmail wa watu,majira ya saa
moja asubuhi tayari alikuwa kwenye gari la KIMOTCO ninalotoka Arusha kwenda
Musoma kwa kupitia Mugumu Serengeti,kitu kinachoitwa hofu moyoni hakikuwepo
hata kwa mbali,ndani ya kipochi chake kidogo alikuwa na pesa taslimu za
kitanzania shiling laki mbili zikisindikizwa na kadi ya viza ya CRDB iliyokuwa
na uwezo wa kutoa shiling laki tano kwa siku mara nne yaani milioni mbili
zilikuwa zimehfadhiwa katika acount yake ya akiba.Mamaa wa shughuli (Eveline)
alikuwa pembeni ya Reshmail,hofu kwake haikuwepo wala hakuiwaza tayari alikuwa
mzoefu wa mambo hayo."Eveline yani akili ndo inakuja sasa hivi eti kwa
nini tusingepanda ndege dah! gari linaenda taratibu hilo jaman" alilalama
Reshmail kwa wananch wa kawaida waliomsikia walidhani ni mashauzi na majigambo
ya watoto wa kike
"Mh? shoga ulivyokuwa na hamu ungekumbuka hayo,tutafika
weye acha papara"
Gari lilizidi kuchanja mbuga za ngorongoro kwa kasi ya kawaida
hadi majira ya saa saba tairi chakavu za gari hili zilikuwa tayari kwenye mbuga
za Serengeti,Resh alikuwa macho anatazama safari inavyokwenda huku akihesabu
masaa yanavyokatika kwa kasi huku mwisho wa safari ukiwa haufiki.Eve yeye
alikuwa ameuchapa usingzi huku akiwa amejifunika uso wake kwa kofia yake nyeusi
ambayo vumbi ilikuwa imeibadili rangi yake na kuwa ya ugoro.(Brown).
"Eve Eve Eve,amka uone wewe" Resh alikuwa anamwamsha
kwa fujo."Angalia hii sms imeingia sasa hv" "Resh mazako kaja
unatafutwa uko wap?" jasho jembamba likaanza kumtoka Resh lakin Eve
hakushtuka sana.Walikuwa wametumiwa ujumbe mfupi na mmoja wa viranja."Eve
tumeisha tumeisha"
* * * * * * * *
Ulikuwa mshikemshke wa ghafla pale shuleni mwalimu aliamuru kila
mmoja aje mstarini hata kama ni mgonjwa,viranja walitii amri na kuita wanafunzi
wote kwa haraka hakuna hata mwanafunzi mmoja aliyebaki ndani ya bweni.
Wakiwa hawajui nini kinachoendelea mwalimu wa zamu aliyeitwa
Mwl.Chipeta alikuwa mbele ya wanafunzi waliokuwa kimya kumsikiliza yeye.”Kabla
sijatoa tangazo hili,ni nani anatambua mwanafunzi ambaye hayupo eneo hili?
(Kimya)
"Nani anaumwa na amepewa ruhusa?" (Kimya)
"Kwa hyo wote mpo?" (Ndiooo)
"Haya mchepuo wa H.G.E wote pita mbele" aliamuru
mwalimu Chipeta na kwa haraka wakaanza kujongea mbele."Mamaaaaa,"
ghafla kelele ilisikika kuna mwanafunzi aliyekuwa mgonjwa alikuwa ameanguka
chini kwa sababu ya kizunguzungu.Ustaarabu ukatoweka pale ghafla kila
mwanafunzi akawa anasema lake,mara hivi mara vile. Hata mwalimu Chipeta
alitimua mbio kuelekea kwenye tukio.
Ni wakat huohuo Joyce ambaye alikuwa kiranja alipata mwanya wa
kutuma ujumbe kwa Reshmail kumpa taarifa.
*****
Roho ilikuwa inamdunda Reshmail kwa kasi sana,aliamin kila kitu
kitakuwa wazi na atafukuzwa shule,"Eve watanielewaje wazazi mie mh!
nimerokoroga" alijisemea Reshmail.
"Upo na steringi lazima tushinde haka kavita kadogo"
Eve alimpa moyo wa ujasiri Resh,"Naomba hiyo simu si ina salio
kidogo"
"Imo elfu tatu"Alijibu huku akimpa simu Eve.
"Sihitaji zote hizo natumia shiling 60 tu hapa"Alijibu
kwa jeuri Eve huku akionekana kujiamini zaidi.
"Sasa hyo 60 itafanya nini shogangu au umesema elfu
sitini?"Alitania Resh na wote wakajikuta wanacheka.
"Dakika tano nyingi majibu mazuri yatakuja,chukua simu yako
ikiingia meseji uisome mi nalala bibie tuliza roho yako hii sio movie ya
kihindi eti stering anauwawa,hili picha la kichina stering anachomwa kisu bado
anapona" alimaliza Eve na kushusha kofia yake ikafunika macho.
Ni kama alivyosema dakika tano zilikuwa nyingi sana ujumbe
kujibiwa
"Na ufanye kweli mi narekebisha mambo nyie tanueni kwa raha
zenu na pia kuhusu yule wa H.G.L vipi?" ulisomeka ujumbe."Mungu wangu
amakweli Eve steringi jamani yaani kirahisi hvyo" alijisemea Resh kwa
sauti ya chini akidhani Eve amelala tayari "Futa sms ya huyo mjnga
nitamalizana nae" kwa saut ya kivivu Eve alimwambia Resh.
USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA
USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA
****
Ndege ya Precion Air ilikuwa inaondoka kutoka Musoma kwenda
Dar-es-salaam kupitia Mwanza majira ya saa kumi na moja wakati basi la KIMOTCO
lilifika saa kumi na nusu jioni,Resh aliona akipanda gari anaweza kuchelewa kwa
Adam Mwanza japo hata umbali wa Musoma kwenda Mwanza hakuufahamu."Resh
ndege ya wapi tunapata sasa hv jaman" Eve alimuuliza Resh wakiwa ndani ya
'Teksi’ kutokea stendi kuu ya Musoma maeneo ya Bweri."Tunajaribu steringi
wangu"
"Haya!! utamu na uchungu wa mapenzi mwachie
aliyeyabeba" alitoa fumbo Eveline.
"Dereva dereva zuia kidogo tafadhali" ghafla Resh
alimwomba dreva naye bila hiana akazikanyaga breki bila kuuliza kulikoni. Mbio
mbio Resh akashuka akaanza kutimua mbio kurudi nyuma huku akiwa peku viatu
ameacha garini Eve,Dereva na wananchi wengine wakabaki kumshangaa.
Mwalimu Chipeta aliongoza zoezi zima la kumshughulikia
mwanafunzi aliyeanguka pale mstarini,shule ya Arusha international ilisifika
sana kwa kujali afya za wanafunzi hivyo tukio lile lilisababisha Mwalimu
Chipeta kumsahau kabisa Bi.Gaudencia mama yake Reshmail na kwenda kushughulika
ipasavyo kwenye lile tukio,aliyekuwa ameanguka alikuwa Naomi Holela mwanafunzi
aliyekuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kifua na pale kilikuwa kimembana hasa
kutokana na baridi iliyokuwepo nje. Gari ya shule ilifika haraka Mwalimu
Chipeta na viranja wawili pamoja na 'matron' walimsindikiza Naomi hospitali.
Akiwa ndani gari Mwalimu Chipeta alisikia simu yake ikitoa mlio wa kupokea
ujumbe mwanzoni alipuuzia kutokana na ubize uliokuwa ukimkabili lakini punde
alitoa simu yake na kufungua ujumbe ulioingia
"Niaje ticha mi Wa ukweli nipo na Resh mbali kimtindo kama
vipi rekebisha mambo huko mi nikija nakuletea geto yule Amina wa
H.K.L,niandalie tu mapene yangu" uso wake ulisahau matatizo yote
yaliyokuwa mbele yake,ni muda mrefu sasa tangu Mwalimu Chipeta muhitimu wa
shahada ya elimu ya fasihi andishi katika chuo kikuu cha Dodoma alikuwa
amemfukuzia binti mrembo wa kawaida tu Amina bila mafanikio tegemeo lake
alikuwa ni Eve au Wa ukweli kama walivyomzoea,bila kupoteza muda Chipeta
alifungua sehemu ya ku'forwad' meseji na akaituma kwa Mwalimu.Madege ambaye
wote lao lilikuwa moja,alikuwa ni mwalimu Madege aliyeijibu ule ujumbe na
kuulizia kuhusu yeye na mpango wa kumpata binti wa H.G.L.
"Samahani wewe ndio mama yake na Reshmail "Mwalimu
Madege aliuliza baada ya Bi. Gaude kuingia katika ofisi ya makamu mwalimu wa
zamu .
"Ndio ni mimi baba"
"Kwanza samahan sana kwa usumbufu uliojitokeza"
"Usijali na mimi niwape pole kwa matatizo
yaliyojitokeza hapa"
"Tunashukuru ndio mambo ya shule haya,eeh! mama nimepokea
ujumbe sasa hivi kwamba mwanao yupo katika mbuga za Serengeti ambapo wanafunzi
watano waliofanya vizuri walipelekwa kufanya utalii wa siku tano"
alidanganya mwalimu Madege.
"Jaman huyu mtoto mbona hakuniambia?... baba yake atafurahi
sana akisikia maendeleo ya mwanae"mama Resh alijieleza kwa furaha
iliyozidi wasiwasi aliokuwa nao.
"Tuliwashtukiza hawakuwa na taarifa hata wao wameshangaa
mno" aliendelea kupanga maneno huku akichorachora mezani kwa kutumia
karamu isiyokuwa na wino.
Moyo wa mama Reshmail uliridhika japo mwili ulikuwa na kinyongo
kwa kukosa haki yake. Ilimbidi siku hiyo hiyo afunge safari kurudi jijini Dar
na zawadi alizokuwa amemletea mwanae zikiwa mikononi mwake.
* * * * * *
A.T.M ya N.B.C aliyoiona maeneo ya Nyasho ilimkumbusha kuwa kadi
yake ni 'VISA' inafanya kazi mashine ya A.T.M ya benki yoyote bila kujali macho
ya watu alitimua mbio pekupeku hadi kwenye mashine ambapo kwa bahati nzuri
hapakuwa na foleni na mtandao ulikuwepo "You can withdraw up to 1000000
with your A.T.M card daily N.B.C WE CARE" kijitangazo kwenye kioo cha
mashne kiliibua tabasamu la Reshmail,na bila ajizi akabonyeza chaguo la kutoa
laki tano kwa mikupuo miwili na kutimiza kiasi cha milioni moja, kisha kwa
mwendo wa mbio kama alivyoingia akatoka akisindikizwa na miluzi ya wauza
mitumba wa Nyasho ambayo kwake haikuwa na madhara hata chembe
"Samahani safari yenu imeahirishwa tafadhali hadi kesho
asubuhi!" sauti nyororo ya mwanadada wa mapokezi aliyehusika na masuala ya
Booking aliwaeleza mwanaume mmoja aliyekuwa na mpenzi wake wakitegemea kusafiri
muda mfupi ujao kwenda Mwanza.
Sura zao zilizokuwa na furaha zililegea na kuwa kama watakavyokuwa pindi wakipata wajukuu,"Haiwezekani huu ni upumbavu tena ujinga ujinga ujinga,yani safari yangu inahairishwa ghafla kama vile safari za baiskeli,hapana sipo tayari nas...."
Sura zao zilizokuwa na furaha zililegea na kuwa kama watakavyokuwa pindi wakipata wajukuu,"Haiwezekani huu ni upumbavu tena ujinga ujinga ujinga,yani safari yangu inahairishwa ghafla kama vile safari za baiskeli,hapana sipo tayari nas...."
"shhhhh!!" kwa ishara ya kidole kimoja kuziba mdomo
alinyamazishwa yule baba aliyetaka kuugeuza ukumbi ule uwanja wa mapambano na
matusi. Kwa ishara nyingine yule dada akamwita akasogea pale alipo
akamnon'goneza "Unawaona wale wasichana wawili,mmoja kimada wa mtoto wa
raisi mwingne mtoto wa kamanda wa jeshi ni simu kutoka ikulu,kwa usalama wako
acha kelele" alimwambia huku akimwelekezea walipo Resh na Eve. Bila kuhoji
huku uoga ukimtawala hadhi yake ikashuka haraka haraka akamvuta mkewe
wakaondoka wakawapisha kwa mbali Resh na Eve kama vile wanatema cheche za moto.
* * * * *
Ni kweli nafasi zilikuwa zimejaa lakini pesa iliongea nafasi ya mtu mwingine wakapewa wao tena harakaharaka,huku mtendaji wa jambo hilo akiweka shilingi laki mbili na nusu kibindoni. Huku Resh na Eve wakipata nafasi katika ndege ya Precision Air kiulaini,kwa mara ya kwanza Eve anapanda ndege "Mh! ushoga nao raha wakati mwingine” alijisemea wakati muhudumu wa ndani ya ndege akitoa maelekezo madogomadogo.
Ilikuwa kama safari ya kutoka Kimara Dar kwenda Mbagala,tayari walikuwa jiji la Mwanza
* * * * *
Ni kweli nafasi zilikuwa zimejaa lakini pesa iliongea nafasi ya mtu mwingine wakapewa wao tena harakaharaka,huku mtendaji wa jambo hilo akiweka shilingi laki mbili na nusu kibindoni. Huku Resh na Eve wakipata nafasi katika ndege ya Precision Air kiulaini,kwa mara ya kwanza Eve anapanda ndege "Mh! ushoga nao raha wakati mwingine” alijisemea wakati muhudumu wa ndani ya ndege akitoa maelekezo madogomadogo.
Ilikuwa kama safari ya kutoka Kimara Dar kwenda Mbagala,tayari walikuwa jiji la Mwanza
"Eve rushwa tamu wewe,naamini haitaisha ona sasa tupo
Mwanza tayari" Resh alimwambia Eve wakati wanasafisha macho yao wajue nini
cha kufanya baada ya kushuka kutoka kwenye ndege.
"Hoteli yenu ni nzuri?" Eve alimuuliza muhusika aliyekuwa ndani ya kigari kidogo kilichoandikwa Millenium Hotels kilichokuwa hapo kwa lengo la kutafuta wateja wanaotua na ndege uwanjani hapo,"Ni nzuri sana hautajuta kuwa pale.”
"Hoteli yenu ni nzuri?" Eve alimuuliza muhusika aliyekuwa ndani ya kigari kidogo kilichoandikwa Millenium Hotels kilichokuwa hapo kwa lengo la kutafuta wateja wanaotua na ndege uwanjani hapo,"Ni nzuri sana hautajuta kuwa pale.”
"Mh! haya,Resh twende giza linaingia" Eve alimwita
Resh wakajitoma ndani ya gari na safari ikaanza.
"Darling umetoka kwenye michezo tayari pole mpenzi" ulikuwa ujumbe mfupi kutoka kwa Adam kuja kwa Resh,tabasamu pana likameza mdomo wake looh! lilikuwa tabasamu lililoelezea furaha ya moyo.
Adam alituma ujumbe huo akijua Resh yupo shuleni tena ilikuwa siku ya michezo ambayo Resh alipenda kushiriki hasahasa mpira wa kikapu.
"Mamaaaaa!!"Resh alipiga kelele ghafla gari ikayumba huku na huko,dereva akajaribu kwa uwezo wake wote kuirudisha barabarani "Paaaa!!" mlio mkubwa ukasikika.
"Darling umetoka kwenye michezo tayari pole mpenzi" ulikuwa ujumbe mfupi kutoka kwa Adam kuja kwa Resh,tabasamu pana likameza mdomo wake looh! lilikuwa tabasamu lililoelezea furaha ya moyo.
Adam alituma ujumbe huo akijua Resh yupo shuleni tena ilikuwa siku ya michezo ambayo Resh alipenda kushiriki hasahasa mpira wa kikapu.
"Mamaaaaa!!"Resh alipiga kelele ghafla gari ikayumba huku na huko,dereva akajaribu kwa uwezo wake wote kuirudisha barabarani "Paaaa!!" mlio mkubwa ukasikika.
*******************
Adam alipokea ujumbe kutoka kwa Reshmail akiwa maeneo ya
kijiweni barabara ya lami kuelekea chuo kikuu cha mtakatifu Augustino,kupitia
shule ya wasichana ya Ngaza.Adam alikuwa pamoja na rafiki yake (Huha) katika
pikipiki ya rafiki yao aliyekuwa amewaazimisha wazungukiezungukie maeneo.
"Huha hebu endesha twende hapo Nyegezi kona kuna mtu nataka
kuonana naye mara moja" Adam alimwomba Huha.
"Tayari Halima ametuma meseji mwambie hatuna mafuta atufate na gari yake bwana" Alitania Huha huku akianza kuiondoa pikipiki taratibu
"Tayari Halima ametuma meseji mwambie hatuna mafuta atufate na gari yake bwana" Alitania Huha huku akianza kuiondoa pikipiki taratibu
"Ungejua hata
usingesema wewe twende ukajionee maajabu ya mwaka" alijibu Adamu huku
pikipiki ikizidi kushika kasi.
Ndani ya dakika tano tayari walikuwa Nyegezi kona ambapo Huha alipaki pembezoni kidogo na barabara iendayo stendi kuu ya Nyegezi jijini Mwanza,Adam alielekea dukani kununua vocha,na Huha akasogea pembeni kidogo aweze kuvuta sigara yake.
USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA
ITAENDELEA....................
Ndani ya dakika tano tayari walikuwa Nyegezi kona ambapo Huha alipaki pembezoni kidogo na barabara iendayo stendi kuu ya Nyegezi jijini Mwanza,Adam alielekea dukani kununua vocha,na Huha akasogea pembeni kidogo aweze kuvuta sigara yake.
ITAENDELEA....................

No comments