Askofu Gwajima Afunguka Mapya Aliyofanyiwa Polisi,Adai Walitaka Kumchoma Sindano....!!!
Askofu wa kanisa la ufufuo na uzima, Josephat Gwajima ameieleza mahakama
ya hakimu mkazi Kisutu kuwa ofisa wa jeshi la polisi alitaka kumchoma
sindano bila ridhaa yake wakati alipolazwa kwenye hospitali ya polisi
Oysterbay.
Askofu Gwajima ameyasema hayo wakati akiongozwa na wakili wake Peter
Kibatala alipokuwa akitoa utetezi katika kesi ya kushindwa kuhifadhi
silaha inayomkabili na wenzake watatu, mbele ya hakimu mkazi mfawidhi,
Cyprian Mkeha.
Mbali ya Gwajima washtakiwa wengine ni mfanyabiashara anayedaiwa kuwa
mlinzi wake, George Mzava, msaidizi wake, Yekonia Bihagaze na mchungaji
Georgey Milulu ambao wanakabiliwa na kosa la kumiliki silaha isiyokuwa
yao.
Katika utetezi wake, Gwajima alibainisha kuwa machi 27, 2015 anakumbuka
alikuwa safarini kuelekea Arusha kwenye kikao cha maaskofu, ambapo
aliondoka jijini Dar es Salaam, machi 26,2015.
Alieleza kuwa wakati alipokuwa njiani kuelekea Arusha aliona taarifa
kwenye mtandao wa kijamii kuwa askofu Gwajima anatafutwa na jeshi la
polisi.
Alieleza kuwa alishangaa kuiona taarifa hivyo, hivyo akafika hadi Arusha
lakini alishindwa kushiriki katika mkutano huo badala yake alianza
safari ya kurudi jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kwenda kwenye kituo
kikuu cha polisi kanda ya Dar es Salaam kwa ajili ya kuripoti.
Gwajima alibainisha kuwa alifika jijini Dar es Salaam ambapo alikwenda
kituoni hapo na kukutana na ofisa mpelelezi wa kanda hiyo na baada ya
muda alianza kuhojiwa, wakati mazungumzo yakiendelea kulikuwa na mtu
aliyekaa nyuma yake akisoma gazeti ambapo kulikuwa na kitu kikimpalia.
Ameeleza kuwa kutokana na hatua hiyo, alianza kupiga kelele kwamba kuna
kitu kinamkera ndipo ghafla akajikuta amepoteza fahamu na hakujua nini
kilichoendelea, alipopata fahamu alijikuta yupo hospitali ya polisi
Oysterbay ambapo wakati akiwa kitandani alimuona mtu aliyevalia mavazi
ya kipolisi ambaye alikuwa na nyota tatu.
Ambaye alitaka kumchoma sindano lakini alikataa na kuanza kubishana naye
kwamba yeye ana daktari wake katika hospitali ya TMJ hivyo apelekwe
huko na kwamba wakati akiendelea kubishana na askari huyo ghafla
alijikuta kapoteza fahamu na alipozinduka alijikuta yupo hospitali ya
TMJ jijini Dar es Salaam.
Baada ya kueleza hayo, hakimu Mkeha ameahirisha kesi hiyo hadi aprili 10
hadi 11, mwaka huu itaendelea kusikiliza ushahidi wa kesi hiyo.

No comments