TAA yashauri somo la urubani lifundishwe kukidhi soko
Mamlaka
ya viwanja vya ndege nchini TAA imekitaka chuo cha usafiri wa anga cha
Regional Aviation cha Dar Es Salaam kuanza kufundisha fani ya urubani
ili kukidhi soko la ndani la wataalam wa fani hiyo.
Akizungumza katika mahafali ya chuo hicho Kaimu Mkurugenzi
Mkuu George Sambali amesema baada ya serikali kusitisha kusomesha
marubani, ndege nyingi za Tanzania zinaendeshwa na marubani wageni
kutokana na upungufu wa marubani wazawa.
Naye Mkuu wa chuo hicho Philemon Kisamo amesema wanafunzi 70 wa fani za uhudumu wa ndege wamehitimu mwaka huu.
chanzo:TBC
Naye Mkuu wa chuo hicho Philemon Kisamo amesema wanafunzi 70 wa fani za uhudumu wa ndege wamehitimu mwaka huu.
chanzo:TBC
No comments