Golden State Warriors watetea taji
Katika
ligi ya kulipwa ya mpira wa kikapu nchini Marekani ya NBA bingwa
mtetezi wa ligi hiyo Golden State Warriors wamefanikiwa kutetea taji lao
la Kanda ya Magharibi
Golden State Warriors watetea taji
Katika ligi ya kulipwa ya mpira wa kikapu nchini Marekani ya
NBA bingwa mtetezi wa ligi hiyo Golden State Warriors wamefanikiwa
kutetea taji lao la Kanda ya Magharibi baada ya alfajiri ya leo kupata
ushindi wa alama 96 kwa 88 dhidi ya Oklohama City Thunder.
Katika mchezo huo namba saba wa kuwania bingwa wa Kanda ya Magharibi, Golden State Warriors kama ilivyo kwa wapinzani wao Oklohama City Thunder walihitaji ushindi wa lazima ili kuwa wababe kutokana na timu hizo kuwa sare ya ushindi wa michezo mitatu kwa kila timu hadi kufikia mchezo wa jana.
Mashabiki zaidi ya elfu 19 waliujaza uwanja wa Oracle Arena mjini Oakland California wakiishangilia timu yao ya Golden State Warriors kwa muda wote.
Nyota mwenye thamani zaidi katika ligi ya NBA kwa misimu miwili mfululizo Stephen Curry alifunga alama 36 na kucheza Rebounds 5 huku Kley Thompson akifunga alama 21 na kuwazidi kete nyota wa Oklohama City Thunder, Kevin Durant aliyefunga alama 27 na Rusel Westbrook aliyefunga alama 19 katika mchezo huo.
Kwa ushindi huo sasa Golden State Warriors watacheza na mahasimu wao wa msimu uliopita Cleveland Cavaliers katika fainali ya NBA kwa msimu huu, ambapo mchezo wa kwanza baina ya timu hizi utachezwa alfajiri ya Ijumaa Juni 3 katika uwanja wa Oracle Arena mjini Oakland California.
CHANZO:TBC

No comments