• Breaking News

    Mkwasa azungumzia AFCON


    Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, Charles Mkwasa amesema mchezo dhidi ya Misri utakuwa ni fainali ya kuamua taifa litakalofuzu kucheza katika fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika -AFCON mwakani kutoka kundi G
    Kocha Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania, Charles Mkwasa
    Mkwasa amesema Misri wanahitaji sare ili wafuzu kwa fainali hizo, lakini hawataipata kupitia mgongo wa Taifa Stars.
    Misri inaongoza kundi G ikiwa na alama saba, ikifuatiwa na Nigeria wenye alama mbili huku Taifa Stars ikiwa na alama moja na hivyo inahitaji kuifunga Misri ili kufufua matumaini ya kufuzu kwa fainali hizo za AFCON.
    Taifa Stars itamaliza mechi zake za kufuzu kwa fainali za AFCON 2017 kwa kucheza na Nigeria mwezi September mwaka huu mjini Abuja.

    CHANZO:TBC

    No comments

    Post Top Ad