• Breaking News

    Fahirisi DSE yapungua


    Fahirisi za sekta ya viwanda katika soko la hisa la Dar Es Salaam, DSE zimepungua kwa alama 2.72 wiki iliyopita kutoka alama 36.26 wiki iliyotangulia
    Meneja Biashara na Masoko wa soko hilo, Patrick Mususa
    Meneja Biashara na Masoko wa soko hilo Patrick Mususa amesema fahirisi hizo zimeshuka kutokana na kushuka kwa bei za hisa za kampuni ya TOL kwa asilimia 3.61, kampuni ya TCCL kwa asilimia 3.03 na kampuni ya sigara ya TCC kwa asilimia 0.83.

    Ameongeza kuwa fahirisi katika sekta ya huduma za kibenki na fedha pia imeshuka kwa alama 10.36 baada ya  hisa ya benki ya CRDB kushuka bei  kwa asilimia 1.33.

    chanzo:TBC

    No comments

    Post Top Ad