Hii Inaitwa Bampa Tu Bampa..Kiongozi wa Korea Kaskazini Amjibu Trump ..Awaandaa Makombandoo Wake Tishio Kuikabili Marekani..!!!
KIONGOZI wa Korea Kaskazini, Kim Jong Un ameanika kikosi chake maalumu cha kijeshi kwa mara ya kwanza mwishoni mwa wiki hii, kama hatua ya makusudi ya kumwonesha Rais wa Marekani Donald Trump uwezo wake kijeshi.
Kikosi hicho chenye askari waliofunzwa barabara kilipita mitaani jijini
hapa Jumamosi wakiimba nyimbo za kizalendo huku wakiwa wamekumbatia
bunduki zao zenye uwezo pia wa kurusha mabomu.
Askari hao wanaosemekana kuwa na vifaa bora vya kivita ndani ya Jeshi la
Watu wa Korea, walivalia pia miwani ya kuonea usiku iliyofungwa kwenye
kofia zao za chuma huku bunduki zao zikining’inia vifuani.
“Mara tu Kamanda Mkuu Kim Jong Un atakapotoa amri, watasonga mbele kwa
lengo la ‘kuuchoma mkuki moyo wa adui kwa kasi ya radi juu ya Mlima
Paektu (kilele kirefu kuliko vyote nchini)’,” mtangazaji wa televisheni
ya Taifa alisikika akitangaza.
Kujitokeza kwa kikosi hicho kwenye sherehe za Siku ya Jua mwishoni mwa
wiki, kulikuja huku kukiwa na msuguano na Marekani na Rais Trump ambaye
amekataa kukanusha mpango wake wa kuishambulia Korea Kaskazini kabla
Rais Kim hajabonyeza kiwambo cha kufyatulia makombora ya nyukilia.
Vikosi maalumu nchini viko tayari kulinda nchi hii dhidi ya majeshi ya
Marekani, ambayo yanafanya mazoezi ya kumng’oa madarakani Kim mara
mapigano yatakapoanza, mchambuzi wa shirika la habari la Yonhap nchini
anadai.
Taarifa ya makao makuu ya Jeshi la Marekani – Pentagon, iliwaelezea
wanajeshi hao wa Korea Kaskazini kama miongoni mwa waliopewa mafunzo
mazuri, wenye vifaa bora, wanaolishwa vizuri na wenye motisha ya hali ya
juu ndani ya Jeshi la nchi hii, CNN iliripoti.
Ilisema kikosi hicho kisiochoonekana mara kwa mara, kinachosemekana
kuendesha operesheni za siri nchini, kinaonekana kuandaliwa kwa ajili ya
operesheni nzitonzito na kujilinda dhidi ya mashambuilizi kutoka nje.
Taarifa hiyo inaendelea kusema, kwamba vikosi hivyo maalumu huendesha
mambo yao katika vitengo maalumu, ikiwa ni pamoja na utambuzi,
mashambulizi ya angani na ya majini, makomando na utaalamu mwingine wa
kijeshi.
Ilibasihiri pia, kwamba Korea Kaskazini imedhamiria kuendesha mapigano
ya masafa marefu, ikitumia makombora ya nyukilia yenye uwezo wa
kuishambulia Marekani moja kwa moja.
No comments