Bungeni: Serikali Kuanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa Ili kuwasaidia Wasanii
Wizara
ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo iko katika mchakato wa kuanzisha
“Mfuko wa Maendeleo ya Sanaa” ambao una dhima kubwa ya kusaidia kuinua
kipato, kuongeza tija na weledi kupitia utaratibu wa upatikanaji fedha
utakaowekwa ili kuwawezesha wasanii kuzalisha kazi bora za sanaa zenye
kukidhi viwango vya masoko ndani na nje ya nchi.
Naibu
Waziri wa Wizara hiyo, Annastazia Wambura ameeleza hayo wakati akijibu
swali la Mbunge wa Kinondoni, Maulid Said Mtulia aliyeuliza juu ya
mpango wa serikali kuwaongezea vifaa, mitaji na menejimenti vijana
walioamua kujiajiri katika sanaa mbalimbali kama vile maigizo, maonesho
ya mitindo na michezo mbalimbali.
Vilevile
Naibu Waziri Wambura, ameeleza kuwa katika kipindi ambacho mfuko wa
maendeleo ya sanaa unaandaliwa, Serikali inashauri Halmashauri zote
ziwasaidie vijana wanaojishughulisha na sanaa kwa kuwapa mikopo yenye
masharti na riba nafuu kwa ajili ya mitaji kutoka kwenye asilimia 10 ya
mapato ya kila Halmashauri kwa kuwa sanaa ni chanzo kikubwa cha ajira
kwa vijana kwa sasa.

No comments