Bungeni: Billioni 1.5 Zatolewa Mikopo Kwa Vijana.
Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma
Serikali
kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana imetoa mikopo yenye thamani ya
Shillingi Billioni 1.5 kwa vikundi vya vijana 129 katika Halmashauri
mbalimbali nchini.
Hayo
yamebainishwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Kassim Majaliwa alipokuwa akitoa hotuba kuhusu mapitio na mwelekeo wa
kazi za Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi
yake kwa mwaka wa Fedha 2017/2018.
“Serikali
inaendelea na azma yake ya kuwawezesha vijana kujikwamua kiuchumi kwa
kutoa mikopo yenye riba nafuu”’ Alisisitiza Mhe. Majaliwa.
Aidha
, Mamlaka za Serikali za Mitaa kupitia mapato yake ya ndani zimetoa
Shillingi Billioni 4.6 ikiwa ni mikopo yenye masharti nafuu kwa vikundi
vya vijana 2,356 na hatua hizi zimekwenda sanjari na utengeji wa maeneo
maalum yenye jumla ya ekari 85,603 kwa ajili ya shughuli za vijana za
Kilimo, biashara ndogo ndogo, burudani na michezo.
Katika
mwaka 2017/2018, Serikali itaendelea kusimamia Halmashauri zote nchini
kutenga asilmia 5 ya mapato yao kwa ajili ya vijana na asilimia 5 kwa
wanawake.
No comments