Bungeni: Waajiri Na Waajiriwa Zingatieni Sheria Za Kazi Kuondoa Migogoro Kazini: Majaliwa
Na Raymond Mushumbusi WHUSM Dodoma.
Waziri
Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa ametoa
wito kwa waajiri na waajiriwa wote nchini kuzingatia Sheria za kazi na
kuimarisha uhusiano katika kazi ili kutumia muda mwingi kufanya kazi
badala ya kutatua migogoro kazini.
Ameyasema
hayo alipokuwa akitoa hotuba kuhusu mapitio na mwelekeo wa kazi za
Serikali na makadirio ya mapato na matumizi ya fedha za Ofisi yake kwa
mwaka wa Fedha 2017/2018.
“Niwaombe
waajiri na waajiriwa kuzingatia Sheria za kazi tupunguze migogoro
kazini ili tuweze kuendana na azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya
kufanya kazi” alisisitiza Mhe. Majaliwa.
Ameongeza
kuwa Serikali imefanya utafiti na kubaini kuwa asilimia 58 ya migogoro
ya kikazi inatokana na kutozingatiwa kwa taratibu za kuachishwa kazi kwa
waajiriwa.
Amezitaja Sekta zinazoongoza kwa migogoro ya kazi kuwa ni Usafirishaji,ujenzi,ulinzi,binafsi,elimu,huduma za Hotel na Viwanda.
Katika
kupunguza migogoro mahali pa kazi Serikali imefanya kaguzi na kusimamia
uundwaji wa Mabaraza ya Wafanyakazi na Tume ya Usuluhishi na Uamuzi
imeendelea kutimiza wajibu wake wa kusuluhisha migogoro ambapo katika
kipindi cha Julai hadi Februari 2016 jumla ya migogoro 8,832
ilisajiliwa na kati ya hiyo migogoro 3,319 sawa na asilimia 37.6 ya
migogoro iliyosajiliwa imesuluhishwa.

No comments