Tarime: Mkurugenzi Awatumbua Watumishi Wawili....Aapa Kumuwajibisha Yeyote Ataripotiwa wa Utovu wa Maadili
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Tarime, Elias Ntiruhungwa
amewasimamisha kazi watumishi wawili wa halmashauri hiyo mbele ya kikao
kwa madai ya kushindwa kufuata maadili ya kazi.
Waliosimamisha
kazi ni, Jeveryson Kaguna kwa madai ya kushindwa kuandaa taarifa za
watumishi kwa wakati zilizokuwa zinahitajika Ofisi ya Rais, zikiwamo za
kupandisha madaraja na ongezeko la mishahara.
Mwingine
aliyesimamishwa ni muuguzi wa Hospitali ya Wilaya ya Tarime, Kegosa
Nega kwa madai ya kuwatukana wagonjwa hospitalini, utoro kazini na
ukaidi.
Mkurugenzi huyo aliwasimamisha kazi katika kikao cha watumishi wa halmashauri alichokiitisha kwa ajili ya kuwakumbusha wajibu wao na kufuata maadili ya kazi.
Mkurugenzi huyo aliwasimamisha kazi katika kikao cha watumishi wa halmashauri alichokiitisha kwa ajili ya kuwakumbusha wajibu wao na kufuata maadili ya kazi.
“Kuanzia
sasa ninamsimamisha kazi ofisa utumishi kwa uzembe wa kushindwa kuandaa
taarifa iliyokuwa inahitajika Ofisi ya Rais mwezi uliopita. Tuliambiwa
tuandae majina ya watumishi wanaotakiwa kupanda madaraja waongezewe
mishahara na kueleza mahitaji ya watumishi.
“Lakini
hajaandaa na nilikuwa namkazania kila mara sasa sijui kama watu
watapandishwa madaraja maana muda umeisha taarifa hazijakwenda,” alisema.
Kuhusu
kusimamishwa kazi kwa muuguzi, alisema alikaidi agizo la mkubwa wake wa
kazi la kumsaidia mgonjwa aliyekuwa amebebwa kwenye kitanda kumsukuma
kumpeleka wodini.
Alisema
hospitali ya wilaya imekuwa ikilalamikiwa kuwa baadhi ya watumishi
hutoa kauli chafu kwa wagonjwa na kupokea rushwa kutoka kwa wagonjwa.
Alisema mtumishi yeyote atakayeripotiwa kwa vitendo vya uvunjifu wa maadili atamuwajibisha.
Alisema mtumishi yeyote atakayeripotiwa kwa vitendo vya uvunjifu wa maadili atamuwajibisha.
“Mtu anakwenda kazini kwa muda anaotaka yeye halafu ni wa kwanza kutoka kazini,” alisema Ntiruhungwa.
Mratibu Elimu Kata ya Nyamisangura, Emanuel Mwihechi alisema suala hilo la watumishi kupandishwa madaraja ni muhimu, lakini kwa halmashauri ya mji limekuwa ni kero kwa watumishi kucheleweshewa madaraja.

Katibu
Tawala wa Wilaya ya Tarime, John Marwa aliwataka watumishi wote wa
Serikali kutekeleza wajibu wao kwa kuzingatia sheria na taratibu za kazi
ili kuepuka matatizo yanayoweza kuzuilika.

No comments