Kahama: Mkuu Wa Wilaya Awapiga Marufuku Walimu Kuzuia kuandikisha Wanafunzi Kisa Vyeti vya Kuzaliwa
Mkuu
wa Wilaya ya Kahama, Fadhili Nkurlu amewapiga marufuku walimu wakuu wa
shule za msingi na sekondari kuzuia kuandikisha wanafunzi wa kidato cha
kwanza na darasa la kwanza hadi wawe na vyeti vya kuzaliwa.
Nkurlu
alitoa agizo hilo baada ya baadhi ya wazazi na wanafunzi kufika ofisini
kwake kusaka vyeti na wengine kulalamika kitendo cha walimu kuwazuia
kuanza kidato cha kwanza.
“Ni
marufuku kwa mwalimu yeyote au kiongozi kuzuia wanafunzi kuandikisha
kwa madai ya cheti cha kuzaliwa kama wanataka kujiridhisha wapate barua
kutoka kwa mwenyekiti wa kitongoji au watendaji wa kijiji na siyo cheti
hicho,” alisema Nkurlu.
Mmoja
wa maofisa elimu kutoka Halmashauri ya Mji wa Kahama, Aruko Lukolela
alisema agizo la mkuu wa wilaya litatekelezwa mara moja.

No comments