• Breaking News

    Lindi haina tatizo la chakula

    Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi
    Mkuu wa mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi amesema mkoa huo hauna tatizo la chakula na kutoa rai kwa wananchi kutunza chakula kilichopo na kulima mazao yanayostahamili ukame.

    Zambi amesema hayo baada ya kukagua hali ya upatikanaji wa chakula katika soko kuu la wilaya ya Nachingwea na kubaini kuwepo kwa chakula cha kutosha.

    Akizungumza na wafanyabiashara wa nafaka katika soko kuu la wilaya ya Nachingwea katika siku yake ya kwanza ya ziara yake wilayani humo, Zambi amesema mkoa huo una akiba ya kutosha ya chakula.

    Amewasihi wananchi wa mkoa huo kutunza chakula kilichopo kwa uangalifu na kuwataka kutumia fedha walizopata kutokana na mauzo ya korosho kununua chakula badala ya kulalamika njaa.

    No comments

    Post Top Ad