NAMNA YA KUFICHA DRIVE ZISIONEKANE
Unapo-click icon ya Mycomputer kwenye computer yako utaona screen ambayo ina icon zifuatazo
(C:)Local Disk , (D:)Local Disk , na (E:)Local Disk .Unaweza ku-hide(kuficha)
local disk D, na local disk E isionekane pindi mtu mwingine atapofungua computer yako.Lakini huwezi ku-hide local disk C kwa sababu program zote zinazoload wakati computer inawake hukaa kwenye local disk C ,na endapo utajaribu kui-hide command hazitakubali.Sasa kama unataka kuhide local disk E,isionekane fuata maelekezo yafuatayo
1.click startbutton iliyopo kwenye desktop, run, halafu andika neno cmd au command,baada ya hapo press enter..{black screen itafunguka hii kitaalamu huitwa DOS au Disk Operating System)
2.Andika neno Diskpart halafu press enter
Nb: Baadhi itataka uallow access click allow na command nyingine yenye neno diskpart itafunguka (Tutaendelea kwa kutumia hii)
3.Andika maneno List Volume halafu press enter
4.Andika maneno select volume E halafu press enter
5.Andika maneno remove letter E halafu press enter
local disk E haitaonekana ,itakuwa hidden tayari
KU-UNHIDE LOCAL DISK AMBAYO UMEI-HIDE FUATA MAELEKEZO YAFUATAYO
1.click startbutton iliyopo kwenye desktop, run, halafu andika neno cmd au command,baada ya hapo press enter..{black screen itafunguka,screen hii kitaalamu huitwa DOS au Disk Operating System)
2.Andika neno Diskpart halafu press enter
3.Andika maneno list volume halafu press enter
Nb: Unaona ya kuwa ile iliyo hidden itakuwa na star kwa nyuma na haina letter kwa sababu tuliitoa..
Angalia namba yake kwa hapa yakwetu ni 3
4.Andika maneno select volume 3 halafu press enter(Hapa tunatumia namba badala ya herufi, namba italingana na disk unayotaka kuirudisha)
6.Drive yako itakuwa imerudi tayari…
No comments