• Breaking News

    Kurudisha Email Zilizofutwa

      Image result for email
    Kwa siku zinatumwa na kupokelewa barua pepe (E-mail) zaidi ya bilioni 205 kupitia mtandao wa Gmail. Namba hii kubwa ya barua pepe inapatikana kwa kuwa watu wamejiandikisha katika vitu mbalimbali kama vile mitandao tofauti...

     tofauti kwa kutumia  barua pepe (Gmail) zao.

    Kutokana na kuwa watu wanapokea barua pepe nyingi sana kwa siku, inakua ni vigumu sana kuzisoma zote na hata pia kuzipangilia. Saa zingine inawabidi kufuta barua pepe nyingi walizopokea kwa mkupuo, na pia inaweza tokea zile zenye umuhimu na zenyewe zikafutwa bila kukusudia. Hili kama likikutokea tunakupa ufumbuzi.

     MUDA WA KUFUFUA
    Kwanza kabisa jambo la muhimu kujua ni kwamba barua pepe zote zilizofutwa huwa zinakaa katika folda linasloitwa ‘Trash‘. Maisha ya barua pepe katika folda hilo ni siku 30 (mwezi) tuu. Baada ya hapo barua pepe hiyo itafutika moja kwa moja.Na baada ya hapo hautakuwa tena na uwezo wa kuweza kuifufua barua pepe hiyo.
    NJIA ZA KUFUFUA BARUA PEPE
    • Fungua akaunti ya Gmail kwa kutumia kompyuta
    • Ikishafunguka nenda katika kibox cha ku ‘search’ pale juu na kisha andika “in:trash” kisha bofya Enter.
    Andika “in:trash” Katika Kibox Cha Kutafuta
    • Fungua barua pepe ambayo unataka kuifufua
    • Click‘ katika sehemu ya ‘Move To‘ na kisha chagua ‘Inbox
    Nenda katika ‘Move To’ na kisha chagua ‘Inbox’
    Mara tuu ukishamaliza fanya hivyo moja kwa moja barua pepe yako inatolea katika ‘trash‘ na kwenda moja kwa moja katika folda la ‘Inbox’

    Ushauri:
    Badala ya kufuta (delete) barua pepe zako inabidi uziweke katika sehemu ya kumbukumbu (Archive) . Kama una barua pepe ambayo ni ya umuhimu basi haina budi kufanya hivyo kwa kumbuka endapo ukifuta barua pepe hiyo baada ya siku 30 itafutika moja kwa moja.
    JINSI YA KUWEKA BARUA PEPE KATIKA ARCHIVE
    • Fungua akaunti ya Gmail
    • Fungua barua pepe unayotaka kuiweka katika kumbukumbu (Archive)
    • Angalia alama ya ‘Archive‘ na kisha ui ‘click‘ kama inavyoonyeshwa kwenye picha hapo chini
    Click Alama Ya ‘Archive’
    • Baada ya hapo barua pepe yako itahifadhiwa.

    Hii ndio namna ya kupangilia barua pepe zako na kuhifadhi zile zenye umuhimu. zile ambazo hazina umuhimu unaweza ukazifuta lakini ikitokea umefuta zile zenye umuhimu kwa bahati mbaya unaweza fanya njia hiyo hapo juu. Ni muhimu kutunza barua pepe wakati mwingine zinakuwa ni ushahidi tosha juu ya jambo fulani (Mfano katika makubaliano). Fuata njia hizi uwe mtaalamu, kama ukikwama usisite kutuandikia katika sehemu ya comment hapo chini.

    No comments

    Post Top Ad