Kampuni ya kufua umeme ya IPTL imesema
haiitambui benki ya Standard Chartered – Hong Kong kama mdai wao wala
haina haki ya kupata malipo yoyote kwa niaba yao.
Kampuni hiyo inaunga mkono hatua ya
Tanesco kukata rufaa katika mà hakama ya ICSID kwasababu hukumu
iliyotolewa ina mapungufu mengi kisheria.Mwanasheria wa IPTL, Joseph Makandege amesema watu wasifanye makosa kuilipa benki hiyo Kwa sababu wanataka kutapeli.
“Hii benki ya Standard Chartered
haistahili kulipwa fedha yoyote kwa niaba yetu. Hatuwatambui kama wadai
wetu, ndiyo maana wanakimbia mahakama za ndani na kwenda nje.”
No comments