JARIDA mashuhuri duniani la Forbes,
limezitaja ndege aina ya Bombardier Dash8 Q400, ambazo tayari Tanzania
imezinunua kuwa ni zenye usalama, zinazotumia mafuta kidogo. Limetabiri
kuwa zitakuwa nguzo muhimu kwa usafiri wa bei nafuu kwa nchi mbalimbali.
Kwa mujibu wa makala iliyochapishwa na
jarida hilo ikiwa na kichwa cha habari “Can Bombardier’s Q400 Save
Regional Air Service in the US?”, mwandishi anafafanua faida ya ndege
hizo, ikilinganishwa na ndege nyingine zinazofanya usafiri wa ndani
nchini Marekani.“Bombadier
ina kasi nzuri na ya kutosheleza mahitaji ya safari za ndani kwa
kiwango cha kuwa na faida zaidi kibiashara, ikilinganishwa na ndege
nyingine za aina yake kama ATR,” linaandika jarida hilo la Forbes.
Aidha, jarida hilo linataja faida
nyingine ya ndege hizo kuwa ni uwezo wa kutumia mafuta kidogo, jambo
litakalosaidia kupunguza gharama za usafiri huo wa ndege nchini kwa
wasafiri wa ndani. Jarida hilo linafafanua kuwa kiwango kidogo cha
mafuta, kinachotumiwa na ndege hizo, kunazifanya kuwa na ufanisi wa
asilimia kati ya 48 mpaka 50 zaidi ya ndege nyingine.
Forbes linasisitiza kuwa kutokana na
gharama za matengenezo kupanda na gharama nyingine za uendeshaji,
ikiwemo mishahara mizuri kwa marubani, kuna uwezekano mkubwa kwa
Bombardier kuendeshwa kwa bei rahisi na ikauza tiketi kwa bei rahisi
zaidi kuliko ndege nyingine.
“Kwa sasa tunakadiria kuwa ndege aina
ya Bombardier, ndizo zitakuwa mbadala na zitashika njia nyingi za ndani
(Marekani) kwa kiasi cha asilimia 50 hadi 60 na zitasaidia kurejesha
usafiri uliositishwa kutokana na gharama kubwa kwa ndege nyingine katika
viwanja takribani 20,” linafafanua jarida hilo.
No comments