RAIS John Magufuli amewashukuru
viongozi na waumini wa Kanisa la Anglikana na madhehebu mengine, kwa
kuendelea kuliombea Taifa na kudumisha amani ma utulivu.
Alisema hayo jana alipoungana na
waumini wa Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano, Dar es Salaam,
kusali ibada ya Jumapili ya kuadhimisha Siku ya Bwana ya 19 baada ya
Pentekoste.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana
na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Ikulu, Gerson Msigwa, Rais aliongozana
na mkewe, Mama Janeth. Alisema Rais wakati akizungumza na waumini wa
kanisa hilo baada ya kumalizika kwa Ibada, aliwashukuru viongozi na
waumini wote nchini kwa kuendelea kuliombea Taifa.
Rais Magufuli alisisitiza kuwa viongozi
wa dini, wanafanya kazi kubwa na muhimu katika Taifa na kwamba
watanzania wote bila kujali dini zao, itikadi za kisiasa, makundi na
kada zao, wana wajibu wa kuungana na viongozi hao ili nia hiyo njema
iendelee kufanikiwa.
“Ninawashukuru kwa sababu mnaendelea
kuliombea Taifa hili, ninawashukuru kwa sababu siku zote mmekuwa mkipiga
magoti na kumtanguliza Mungu mbele, ninawashukuru kwa sababu mnaendelea
kuombea amani ya nchi yetu na upendo udumu ndani yetu sisi sote.
No comments