SIMULIZI: FACEBOOK SEHEMU 02
SEHEMU YA 01
ILIPOISHIA...................
"Mwanangu nimekuunga na wewe namba yako ya siri ni..,.." hata kabla Huha hajamaliza adam akamkatisha "Nini? huo upumbavu wako sitafanya kamwe bro" ..."Hv kwan inakuwaje huo upuuzi" Adam akajikuta anauliza baada ya kuwa amevaa nguo zake "Hii kitu inaitwa FACEBOOK,yan adam ukijiunga wewe hutoki na utakuwa nayo bize kweli" Adam alisikiliza kwa makin japo alijidai kufanya dharau machon,Huha hakujali aliendelea kutoa somo had Adam akapata mwanga,"Mh. Sidhan kama itanivutia bt i wil try". Alijisemea adam wakat anachukua simu yake.
USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA
INAENDELEA......
Tabia ya Adam ilikuwa imebadilika ghafla ni Adam na
facebook,facebook na yeye,iwe barabaran,club,lecture room,hostel yani kasoro
mskitini tu ndio Adam aliweza kuhfadh simu yake.Sio Huha wala rafiki yake
yeyote aliyejua nini zaid ya facebuk kimemuathiri adam wa watu.Hakumuazima tena
Huha simu,hakutaka mazoea na wasichana ni yeye na simu yake tu!! "Adam mbona
washkaji wanalalamika eti wanakuomba urafiki facebook unachomoa? siku moja Huha
aliamua kumuuliza Adam baada ya kuona tabia yake imekuwa ya ajabu mno
kupindukia."Sitaki that's all".
Ndio jibu fup alilopewa.kisha adam
akajiondokea.Huha akabaki ameduwaa asijue la kufanya,mara ghafla adam akarudi
tena "Huha naomba ukamwambie Halima simtaki,usiniulize kwa nini mwambie
SIMTAKI!" adam alimwambia Huha kana kwamba alimfumania huyo halima.
Mpenz msomaj Halima alikuwa binti matata pale chuon kwa kipind
kile,Adam ndo alipata fursa ya kuangukia penz lake,penz lao chuo kizima
walifahamu,gari ya Halima ilikuwa kama ya Adam..chumba cha Cha Halima
kilipambwa picha na kad za Adam lait na Adam angekuwa anakaa peke yake basi
hata yeye chumba chake kingekuwa had na nguo za ndan za Halima pamoja na pedi
bas tu alikuwa anakaa na Huha.
Huha alibak mdomo waz akijiuliza ni Adam au kivuli chake
kinaongea.Alikuwa Adam sio kivuli.....
Ubize aliokuwa nao mheshimiwa mbunge ulimkosesha raha mkewe
bi.Gaudensia Ogunde,hakuipata haki yake ndoa kwa takribani mwezi mmoja
sasa,mume alikuwa anachelewa kurudi na akirudi anakuwa amechoka sana kutokana
na majukumu mazito ya kiserikali,na ikitokea siku akathubutu kujaribu kutoa
huduma basi alikuwa hamridhish mkewe,taratibu mama akajaribu kuzoea lakini kuna
wakat uvumilivu ulikuwa unamshnda,nyumba nzima alikuwa akiish yeye,mtoto wake
wa kike na msaidiz wa kazi (House girl).
"Mwanangu ni siku ya tatu baba
yako halali nyumbani,najisikia mpweke sana kulala mwenyewe" bi.Gaudensia
alimweleza mwanae kwa unyonge "Pole sana mamii hata mi sipend hyo tabia ya
baba,leo nakuja kulala na wewe mama" alijibu yule binti mwenye miaka 17
akiwa ndio kwanza amemaliza kidato cha nne.Mama hakujibu kitu badala yake
alimkumbatia mwanae kwa sekunde kadhaa kisha akamwachia huku machozi
yakimlengalenga.
****** Reshmail Mtoto wa mwisho na pekee wa kike kati ya watoto wanne wa mbunge wa jimbo la Kinondoni Mheshimiwa Msuruli Haruna,hakupata kujua shida katika maisha yake na urembo aliojaliwa pia hakuufaham kwa sababu hakuwepo wa kumwambia kuwa yeye ni mrembo,kuta na fensi ya sen'gen'ge iliyozunguka mji wao haikumruhusu kutoka nje hovyo hovyo,tofauti na siku ya kwenda msikitini Resh alilazimika kusubiri hadi alipofikisha miaka kumi na nne alipojiunga na kidato cha kwanza katika shule ya st.marry's international ndio alipata wasaa wa kujumuika na wananch wengne wa Tanzania na nchi za jirani,elimu yote ya darasa la kwanza hadi la saba aliipatia katika jumba la kifahari la baba yake.
Mazoea ya kuish maisha ya peke yake peke yake yalimtesa sana Resh kiasi kwamba hadi anamaliza kidato cha nne aliweza kuwa karibu kiurafiki na wanafunzi wachache na weng wao wakiwa wasichana tena watoto wa matajiri na vigogo mbalimbali wa serikali.Kampani kubwa ya Reshmail alikuwa ni mama yake mzazi,yalikuwa ni mazoea makubwa sana lakini yasiyoshangaza,mara nying walikuwa wanatembea pamoja huku wameshkana mikono huku wakifurah sana.
USISAHAU KULIKE PAGE YETU YA FACEBOOK HAPA
Kidato cha tano na sita katika shule ya Arusha international school ndio kwa mara wa kwanza ilimpeleka nje ya jiji la dar-es-salaam.
ITAENDELEA..................

No comments