• Breaking News

    Jurgen Klopp aweka kandarasi ya miaka 6 na Liverpool

    Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp ameweka kandarasi mpya ya miaka sita na mmiliki wa klabu hiyo akisema ingekuwa makosa kutompatia

    kandarasi ndefu.
    Klopp alijiunga na Liverpool mnamo mwezi Oktoba ,baada ya kukubali mkataba wa pauni milioni 15
    ambao umeongezwa hadi mwaka 2022.
    ''Uongozi wake utakuwa muhimu katika kufanikisha malengo yetu'' ,alisema mmiliki wa Liverpool.
    Klopp aliifikisha Liverpool katika fainali ya League Cup pamoja na fainali ya Europa League msimu
    uliopita.
    Raia huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 49 aliisaidia Borussia Dortmund kushinda mataji
    mawili ya Bundesliga pamoja na kucheza fainali ya
    vilabu bingwa Ulaya 2013.

    No comments

    Post Top Ad