• Breaking News

    MOURINHO ATHIBITISHIWA WASAIDIZI MAN UNITED

    WASAIDIZI wa kocha mpya
    wa Manchester United, Jose
    Mourinho wamethibitishwa.
    Msaidizi namba moja
    mwaminifu wa Mourinho, Rui
    Faria amekuwa Kocha
    Msaidizi wa Mashetani hao
    Wekundu.
    Mourinho alikutana kwa mara
    ya kwanza Faria Barcelona
    kabla ya kufanya naye kazi
    klabu ya Uniao de Leiria ya
    Ureno kama kocha wa
    mazoezi ya viungo na
    akaenda naye Chelsea mara
    zote mbili, Inter Milan na
    Real Madrid.
    Kocha Silvino Louro, ambaye
    amekuwa na Mourinho kwa
    zaidi ya muongo mmoja
    kama kocha wake wa
    makipa, pia ametajwa katika
    jopo la makocha wanne
    wasaidizi wa Mreno huyo Old
    Trafford.
    Ricardo Formosinho na
    Carlos Lalin - ambao pia
    wana uzoefu wa kufanya kazi
    na Mreno huyo awali - na
    Emilio Alvarez pia
    wamethibitishwa katika
    benchi la Ufundi pamoja na
    mtathmini, Giovanni Cerra.
    Uthibitisho wa United wa
    benchi hilo la Ufundi unakuja
    baada ya Mourinho kujivua
    lawama za kuondoka kwa
    Ryan Giggs aliyekuwa Kocha
    Msaidizi namba moja
    kwamba hahusiki.
    Katika mkutano wa
    kumtambulisha rasmi
    Jumanne Old Trafford,
    Mourinho alisema kwamba
    ilikuwa ni vigumu kwa winga
    huyo wa zamani wa United
    kubaki kulingana na
    mazingira.

    No comments

    Post Top Ad