Katika kuimalisha kikosi chake Leicester yamsajili mshambuliaji wa Nigeria
Klabu ya Leicester City imemsajili mshambuliaji wa Nigeria Ahmed Musa kutoka CSKA Moscow kwa kandarasi ya miaka 4 itakayogharimu pauni milioni 16.
Southampton,Everton na West Ham walikuwa wakitafuta saini ya mchezaji huyo.
Musa ni mchezaji wa nne kusajiliwa na Leicester baada ya kipa Ron-Robert Zieler ,beki Luis Hernandez na kiungo wa kati Nampalys Mendy.
Mchezaji huyo alijiunga na CSKA mwaka 2012 na
kufunga mabao 54 kati ya mechi 168
alizocheza,na amefunga mabao 11 katika mechi 58
alizochezea Nigeria tangu aanze kucheza mwaka
2010.

No comments