JUA ZAIDI FAIDA ZA PARACHICHI

Parachichi ni tunda
ambalo mti wake hujulikana kisayansi kamaPersea amerikana. Tunda
hili lina aminika kuwa na asili kutoka jimbo la Puebla, bara Amerika ya kusini
kunako nchi ya Mexico. Ushahidi wa kale kabisa, takribani miaka 10000 BC
umeonyesha parachichi lilitumika katika jimbo la Puebla nchini Mexico. Lakini
kutokana na faida nyingi kiafya zipatikanazo kwa ulaji wa tunda hili, tunda
hili sasa hupatikana na kutumika kwa lishe sehemu nyingi duniani hususani
barani Afrika.
Parachichi ni tunda la
pekee ukilinganisha na matunda mengine, kimsingi matunda mengine huwa yana
wanga(carbohydrate) kwa wingi, wakati parachichi lina aina ya mafuta
ambayo yana faida kwa afya.
Aina ya kirutubisho
|
Kirutubisho
|
Kiwango kilichopo
|
Vitamini
|
Vitamini A
|
7ug
|
Vitamini E
|
2.1ug
|
|
Vitamini C
|
10mg
|
|
Thiamine
|
0.1mg
|
|
Niacini
|
1.7mg
|
|
Vitamini B 6
|
0.3mg
|
|
Folic acid
|
81ug
|
|
Madini
|
Kalshamu
|
12mg
|
Phosphorasi
|
52mg
|
|
Magnesiamu
|
29mg
|
|
Potasiamu
|
599mg
|
|
Munyu (Sodium)
|
7mg
|
|
Chuma
|
0.6mg
|
|
Zinki
|
0.6mg
|
|
Shaba
|
0.2mg
|
|
Manganizi
|
0.1mg
|
|
Protini muhimu
|
TRP(Tryptophan)
|
25mg
|
THR(Threonine)
|
73mg
|
|
ILE(Isoleucine)
|
84mg
|
|
LEU(Leucine)
|
143mg
|
|
LYS(Lysine)
|
132mg
|
|
MET(Methionine)
|
30mg
|
|
CYS(Cysteine)
|
27mg
|
|
PHE(Phenylalanine)
|
232mg
|
|
TYR(Tyrosine)
|
49mg
|
|
VAL(Valine)
|
107mg
|
|
ARG(Arginine)
|
88mg
|
|
HIS(Histidine)
|
49mg
|
Parachichi katika
tafiti nyingi limeonekana kuwa na faida katika afya ya moyo. Wagonjwa wa moyo
wamekuwa katika makatazo ya kutumia aina ya mafuta ambayo yamekuwa yakichangia
kuongezeka kwa lehemu katika damu(mafuta hayo kitaalam kama polysaturated
fat), na kuongeza matumizi ya mafuta yasiyoongeza lehemu katika damu (monosaturated
fat). Parachichi ni chanzo kizuri cha mafuta yasiyoongeza lehemu katika
damu. Utafiti unaonyesha kuwa matumizi ya mafuta haya katika parachi
hupunguza lehemu iliyo hatari ( kitaalam kama, Low density lipoprotein),
na huchangia katika ongezeko la lehemu isiyo hatari( High density
lipoprotein).
Madini ya Potasiamu ni
aina ambayo huwa watu hawapati ya kutosha kutoka katika vyakula. Parachichi
lina kiwango kikubwa cha madini ya potassium kuliko ndizi. Tafiti mbalimbali
zimeonyesha kuwa matumizi ya madini haya huambatana na kupungua kwa shinikizo
la damu, shinikizo la juu la damu laweza kupelekea mtu kupata kiharusi,
shambulizi la moyo hata figo kushindwa kufanya kazi.
Parachichi lina
kiwango kikubwa cha fiba. Fiba ni kirutubisho kutoka katika vyakula vya jamii
ya mimea, fiba huwa hazimeng’enywi tumboni lakini huwa zina umuhimu mkubwa
sana, kama kusaidia kupunguza uzito wa mwili, kusaidia urekebishaji wa kiwango
cha sukari mwilini na kupunguza hatari ya kupata magonjwa mengi mwilini. Kuna
aina fulani ya fiba ambazo huwa ni virutubisho kwa ajili ya bakteria wenye
faida tumboni, hii huimarisha kinga ya mwili na kusaidia mwili kufanya kazi
katika kiwango kinachotakiwa. Kwa kuwa parachichi lina kiwango kikubwa cha
fiba, husaidia kuboresha mmeng’enyo na kupata choo katika hali
ya kawaida.
Aina ya mafuta na
virutubisho tulivyoviona awali katika parachichi vinasaidia afya ya ngozi yako.
Husaidia ngozi yako kutokuwa kavu na kuwa na unyevu unaotakiwa na kuifanya
ngozi kuwa laini na yenye afya. Vitamini C husaidia katika kusaidia uponaji
haraka wa ngozi na kujijenga upya kwa seli za ngozi zilizoharibika,husaidia
kujenga elastini na collageni ambazo ni
muhimu katika ngozi. Uwepo wa virutubisho viondoavyo sumu(antioxidants)
katika parachichi kama carotenoidi na vitamini E, hutusaidia kutukinga na
mionzi mikali ya jua, kwa hiyo huzuia makunyanzi katika ngozi na kuifanya ngozi
yako kuwa na mwonekano mzuri wakati wote.
Tunda hili ni lishe
bora kwa wale wenye kisukari. Parachichi lina kiwango kidogo cha sukari
ukilinganisha na matunda mengine. Pia uwepo wa mafuta aina ya ‘monosaturated’ husaidia
kuboresha ufanyaji kazi wa homoni ya insulini, katika urekebishaji wa kiwango
cha sukari mwilini. Faida nyingine ni kuwa Vitamini C katika parachichi
husaidia kuimarisha mishipa ya damu na kuboresha kinga ya mwili ambayo ni faida
kubwa kwa wagonjwa wenye kisukari.
Faida katika afya ya
uzazi ni dhahiri. Parachichi lina Vitamini E ambayo ni “antioxidant”
Potasiamu, Vitamini B6,Vitamini C ambazo hutusaidia kutukinga na magonjwa ya
moyo hata yale ya kisukari. Chochote kile kinachosaidia afya ya moyo pia
husaidia afya ya uzazi. Wanaume wenye magonjwa ya moyo na kisukari huwa tatizo
kubwa la upungufu wa nguvu za kiume.
Parachichi pia
limeonekana kuwa na faida nyingi katika kuboresha afya ya macho, viungo vya
mwili na nyinginezo nyingi. Katika utafiti mmoja uko Marekani, ulionyesha kuwa
watu walao parachichi walionekana kuwa na afya bora ukilinganisha na wale wasiokula
parachichi. Waliokula parachichi hawakupatwa na matatizo ya mmeng’enyo ukilinganisha
na wale wasiokula. Matatizo ya mmeng’enyo huchangia watu kupatwa na magonjwa ya
moyo na kisukari.
Unasubiri nini sasa?
Anza kutumia matunda haya kuboresha afya yako. Unapokwenda sokoni usisahau
kununua parachichi.Faida ni nyingi zitokanazo na ulaji wa tunda hili.
No comments