TUPANDE MITI YA MATUNDA KUKIDHI KIWANGO KINACHOHITAJIKA KWA SIKU.
Kila hatua
utakayochukua ya kula zaidi matunda na mboga mboga, itakusaidia wewe na familia
yako kuwa na afya njema. Hii ni kwa sababu matunda na mboga za majani yana
viini lishe muhimu ambavyo husaidia ufanyaji kazi wa mifumo ya miili yetu na
kutukinga na aina mbali mbali za magonjwa.
Kwa mujibu wa shirika
la afya duniani WHO, ni kuwa ulaji wa angalau gramu 400(pungufu kidogo ya
nusu kilo) za matunda na mboga kwa siku zinatuepusha na hatari ya kupata
magonjwa yanayosumbua jamii nyingi duniani hivi leo. Magonjwa haya zaidi ni
yale yasiyo ya
uambukizi kama kisukari, shinikizo la damu, kiharusi na
mengine mengi. Pia ulaji wa matunda na mboga mboga utatusaidia kupata
viini lishe kama fiba, vitamini, madini katika viwango sahihi
vinavyohitajika kwa siku.
Katika nchi
zinazoendelea ambapo walio wengi wanaishi chini ya dola moja kwa siku, ni
vigumu kuweza kumudu kufikia kiwango kilichopendekezwa na shirika la afya
duniani, lakini hii isitufanye kushindwa kumudu kiwango kilichopendekezwa.
Tunaweza kujitosheleza kwa matunda na mboga za majani kwa kuotesha miti ya
matunda mbali mbali majumbani mwetu, pia kuwa na bustani za mboga mboga. Hii
itatusaidia kuweza kufikia kiwango kinachopendekezwa na shirika la afya WHO na
kuboresha afya zetu.
Ili kuboresha kiwango kinachohitajika cha
matunda na mboga mboga, basi hatuna budi kufanya
yafuatayo:-
·
Tuhakikishe kuwa
nyumbani kwetu hapakosekani bustani za mboga na matunda.
·
Kila wakati hakikisha
katika mlo wako haukosi mboga za majani.
·
Hakikisha haukosi
matunda ya kila msimu, mfano embe, nanasi, chungwa, mastafeli, papai,
fenesi,parachichi na mengineyo mengineyo mengi.
·
Kula aina tofauti za
matunda na mboga za majani.
uambukizi kama kisukari, shinikizo la damu, kiharusi na mengine mengi. Pia ulaji wa matunda na mboga mboga utatusaidia kupata viini lishe kama fiba, vitamini, madini katika viwango sahihi vinavyohitajika kwa siku.

yafuatayo:-
No comments