FAIDA ZA TIKITI MAJI.

Tikiti
maji ni tunda ambalo kisayansi hujulikana kamaCitrullus lanatus katika
familia ya Cucurbitaceae,ambalo mmea wake hutoa maua na humea kwa
kutambaa. Mmea huu ambao hutoa matunda makubwa yaliyo na umbo la tufe au yai,
asili yake ni huko kusini mwa Afrika.
Ushahidi wa kihistoria
ulionyesha kuwa mmea huu ulilimwa huko Misri tangu milenia ya pili BC, na
katika karne ya kumi AD mmea wa tikiti maji ulikuwa umesambaa huko bara Hindi
hata Mashariki ya mbali.Lakini hapo badae ulimaji
wake ulifika huko Ulaya ya kusini na kusambaa duniani kote.Tafiti nyingi zimekuwa zikifanyika kujaribu kuzalisha mbegu za tikiki zenye kukabiliana na magonjwa yashambuliayo mmea huu.
wake ulifika huko Ulaya ya kusini na kusambaa duniani kote.Tafiti nyingi zimekuwa zikifanyika kujaribu kuzalisha mbegu za tikiki zenye kukabiliana na magonjwa yashambuliayo mmea huu.
Ijapokuwa watu wengi
huamini kuwa tikiti maji ni tunda lililo na maji na sukari peke yake, lakini
ukweli ni kuwa tunda hili lina aina nyingi ya virutubisho , mfano vitamini,
madini na viondoa sumu(antioxidants).
Jedwali likionyesha
kiasi cha virutubisho katika gramu 100 za tikiti maji.
Aina ya kirutubisho
|
Kirutubisho
|
Kiwango kilichopo
|
Vitamini
|
Vitamini A
|
28µg
|
Vitamini E
|
0.0 µg
|
|
Vitamini C
|
8.1mg
|
|
Thiamine
|
0.03mg
|
|
Niacini
|
0.2mg
|
|
Vitamini B 6
|
0.045mg
|
|
Folic acid
|
3mg
|
|
Madini
|
Kalshamu
|
7mg
|
Phosphorasi
|
11mg
|
|
Magnesiamu
|
10mg
|
|
Potasiamu
|
112mg
|
|
Munyu (Sodium)
|
1mg
|
|
Chuma
|
0.2
|
|
Zinki
|
0.1mg
|
|
Shaba
|
0.0mg
|
|
Manganizi
|
0.0mg
|
|
Protini muhimu
|
TRP(Tryptophan)
|
7.0mg
|
THR(Threonine)
|
27mg
|
|
ILE(Isoleucine)
|
19mg
|
|
LEU(Leucine)
|
18mg
|
|
LYS(Lysine)
|
62mg
|
|
MET(Methionine)
|
6mg
|
|
CYS(Cysteine)
|
2mg
|
|
PHE(Phenylalanine)
|
15mg
|
|
TYR(Tyrosine)
|
12mg
|
|
VAL(Valine)
|
16mg
|
|
ARG(Arginine)
|
59mg
|
|
HIS(Histidine)
|
6mg
|
Mbali na virutubisho
vilivyoonyeshwa katika jedwali, tunda hili la tikiti maji pia lina viondoa sumu
kamaflavonoids, carotenoids na triterpenoids pia
kiasi kikubwa cha maji,na virutubisho hivi hulifanya tunda hili kuwa na sifa ya
vyakula vyenye faida kubwa mwilini.
Tafiti nyingi
zimeonyesha kuwa, kuongeza matumizi ya vyakula vitokanavyo na mimea kama tikiti
maji,matunda mengine na mbogamboga hupunguza hatari ya kupata magonjwa,
kuboresha maisha na kuongeza umri wa kuishi. Twaweza kuepukana na magonjwa kama
uzito mkubwa(obesity),kisukari na magonjwa ya moyo. Ulaji wa vyakula
hivi humfanya mtu kuwa na afya njema,ngozi yenye afya,nywele na uzito ulio wa
wastani.
Tunda hili lenye lycopene ambayo
ni kiondoa sumu(antioxidant) na ambayo hulipa tunda hili rangi ya
kupendeza iliyo nyekundu au pink, pia hupatikana katika nyanya na matunda
mengine yaliyo na rangi nyekundu.
Tafiti za awali
zimeonyesha kuwa watu walao matunda kama tikiti na mengineyo yenye lycopene kwa
wingi waweza kuwa na nafasi ndogo ya kupata maradhi ya saratani hususani
saratani ya tezi dume. Lakini hapajakuwepo kwa ushahidi ulio thabiti
kuonyesha uhusiano uliopo kati ya saratani ya tezi dume na utumiaji wa
matunda yenye lycopene ili kuweza kutambuliwa na mamlaka za
chakula na tiba.
Katika utafiti mmoja
uliochapishwa mwaka 2013 katika jarida la Kimarekani la shinikizo la
damu,ulionyesha ulaji wa tikiti maji kwa watu wazima walio na uzito mkubwa
uliweza kupunguza shinikizo la damu la aota (aortic BP).

L-citrulline ni aina ya
protini iliyo katika tikiti maji na ambayo hubadilishwa mwilini katika figo na
kuwa protini ijulikanayo kama L-arginine. L-citrulline pia
huongeza utengenezwaji wa nitric oxide,ambayo hufanya mishipa ya
damu kutokukakamaa na kuboresha mzunguko wa damu mwilini na hii ndiyo sababu ya
kupungua kwa shinikizo la damu. Tunda hili limejipatia umaarufu kwa wale walio
katika ndoa,kwa kuwa nitric oxide huongeza pia mzunguko wa
damu katika viungo vya uzazi, kwa hiyo wale walio na tatizo la upungufu wa
nguvu za kiume kwa kiwango kidogo na kati, waweza kufaidika na tunda hili.
Kwa wana michezo ulaji
wa tunda hili au juisi yake ni wa faida kubwa kwa kuwa husaidia kupunguza
maumivu ya misuli na kuondokana na uchovu kwa haraka baada ya mazoezi au
michezo ya kutumia nguvu. Watafiti wanaamini kuwa hii ni kwa sababu ya uwepo wa
protini ya L-citrulline katika tikiti maji.
Tikiti maji ni tunda
muhimu katika kurekebisha mmeng’enyo. Kwa kuwa tunda hili limetengenezwa
na kiasi kikubwa cha maji na fiba husaidia kuondoa matatizo ya kukosa choo (constipation)
na kuboresha mmeng’enyo wa chakula tumboni. Pia kwa kuwa tunda hili lina
asilimia 92 ya maji na madini, huwa ni chaguo zuri kwa wagonjwa wenye upungufu
wa maji mwilini.
Hatari ya kupata
ugonjwa wa pumu ni mdogo kwa wale wanaokula aina fulani ya virutubisho. Katika
moja ya virutubisho hivi ni vitamini C ambayo hupatikana katika aina nyingi za
matunda na mbogamboga likiwemo tikiti maji.
Tikiti maji husaidia
afya ya ngozi kwa kuwa lina vitamini A na C. Vitamini A husaidia katika ukuaji
wa tishu za mwili,zikiwemo ngozi na nywele. Vitamini C husaidia katika
utengenezaji wa kolageni mwilini na husaidia kupona haraka kwa tishu zilizo na
majeraha ikiwemo ngozi.
Tahadhari
Tikiti maji siyo lishe
iliyokamilika peke yake, pia siyo tiba itakayokufanya kuacha kufuata ushauri wa
daktari. Ni vema basi kuhakikisha tunakula mlo ulio kamilika ili kujenga afya
bora. Tunapopata matatizo mbali mbali ya kiafya ni vizuri pia kuonana na wataalamu
wa afya kwa ajili ya utafiti, ushauri na kupata tiba iliyo sahihi.
No comments