• Breaking News

    Wananchi na vyama vya siasa wahimizwa kulinda amani



    Serikali imesema wananchi na viongozi wa vyama vya siasa nchini ni lazima watii sheria ya Jeshi la Polisi ya kutofanya mikutano ya hadhara hadi pale watakaporuhusiwa na jeshi hilo kufanya mikutano hiyo.
    Akijibu swali bungeni mjini DODOMA Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, HAMAD MASAUNI, amesema lengo la kusitisha mikutano ya hadhara ni kuimarisha usalama wa nchi.
    Naye Naibu Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt ASHATU KIJAJI amesema  serikali inawahimiza wafanyabiashara nchini kutumia mashine za EFD ili kuweza  kupata kumbukumbu za mauzo yao na si vinginevyo. Hivyo amewataka wafanyabiashara hao  kwenda kuchukua mashine hizo zinazotolewa bure kwa sasa.
    Wakati huo huo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa- TAMISEMI-,  GEORGE SIMBACHAWENE, amewataka wabunge kuorodhesha miradi  chakavu  na kuipa kipaumbele kwenye bajeti zao ili serikali iweze kuifahamu na kuifanyia kazi.

    No comments

    Post Top Ad