TBC yapokea msaada wa ujenzi wa studio mpya
Shirika la Utangazaji Tanzania TBC limetiliana saini mkataba na mfuko wa mawasiliano kwa wote nchini wa shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa studio mpya
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini TBC Dokta AYUB RIOBA
Shirika la Utangazaji Tanzania TBC limetiliana saini mkataba na mfuko wa mawasiliano kwa wote nchini wa shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa studio mpya ya matangazo ya FM mkoani ARUSHA.
Akizungumza mara baada ya kutiwa saini makubaliano hayo mjini DSM ,Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano nchini Mhandisi PETER ULANGA amesema uamuzi wa kuisaidia TBC umefikiwa ili iweze kuboresha usikivu wa matangazo yake.
Kwa upande wake mkurugenzi mkuu wa Shirika la Utangazaji nchini TBC Dokta AYUB RIOBA ameshukuru kwa msaada huo ambao amesema utaweza kuimrisha usikivu wa TBC na kuhakikisha wananchi wanapata habari zilizo bora.
Dokta RIOBA amesema TBC itaendelea kuboresha usikivu kwa vyombo vyake vyote ili wananchi waweze kuelemika kupitia taarifa mbalimbali zinazotolewa.

No comments