Mtoto wa aliyekuwa waziri mkuu wa PAKISTAN azungumzia kutekwa na AL QAEDA
Mtoto wa aliyekuwa Waziri Mkuu wa PAKISTAN amezungumza kwa mara ya kwanza kuhusu kutekwa nyara kwake na Kundi la AL QAEDA.
ALI HAIDER GILANI
Katika mahojiano na waandishi wa habari, ALI HAIDER GILANI amesema AL QAEDA walimwambia kuwa kutekwa kwake ni hatua ya kulipiza kisasi dhidi ya baba yake.
Watekaji hao walitaka kulipwa fedha na kuachiwa kwa wafungwa wa Kundi la AL QAEDA.
GILANI aliokolewa katika operesheni inayofanywa na MAREKANI na AFGHANISTAN katika Jimbo la PAKTIKA.
Baba wa GILANI alikuwa Waziri Mkuu wakati Kiongozi wa AL QAEDA, OSAMA BIN LADEN alipouawa nchini PAKISTAN.
GILANI amesema alishikiliwa kwa miaka miwili na kukabidhiwa kwa wanamgambo wa TALIBAN nchini PAKISTAN baada ya shambulio la ndege zisizo na rubani kufanya shambulio Kaskazini mwa Jimbo la WAZIRISTAN wakilenga ngome za AL QAEDA.

No comments