• Breaking News

    Rais WA UTURUKI amuomba radhi rais WA RUSSIA

    Rais RECEP TAYYIP ERDOGAN wa UTURUKI amemwandikia barua Rais VLADIMIR PUTIN wa RUSSIA akimuomba radhi kutokana na kuangushwa ndege ya nchi hiyo


    Rais RECEP TAYYIP ERDOGAN wa UTURUKI
    Rais RECEP TAYYIP ERDOGAN wa UTURUKI amemwandikia barua Rais VLADIMIR PUTIN wa RUSSIA akimuomba radhi kutokana na kuangushwa ndege ya nchi hiyo katika mpaka wa UTURUKI na SYRIA.
    Ikulu ya Rais wa RUSSIA imetoa taarifa ikisema kuwa Rais RECEP TAYYIP ERDOÄžAN amemwandikia barua Rais PUTIN akieleza matarajio ya kutatuliwa hali iliyojitokeza katika uhusiano wa nchi hizo mbili baada ya kutunguliwa ndege ya kivita ya RUSSIA.
    Katika barua hiyo Rais ERDOÄžAN ametuma tena salamu za rambirambi kwa familia ya rubani wa ndege hiyo na kueleza kusikitishwa na tukio hilo.
    Uhusiano wa RUSSIA na UTURUKI uliharibika Novemba mwaka jana baada ya UTURUKI kutungua ndege ya kijeshi ya RUSSIA katika anga ya SYRIA.

    UTURUKI ilidai kuwa ndege hiyo ya kijeshi iliingia katika anga yake.

    No comments

    Post Top Ad