Jeshi la Polisi lakamata Bunduki 4
Polisi Mkoani TABORA imekamata Bunduki NNE zilizokuwa zinatoroshwa ikiwa ni siku kadhaa baada ya Mkuu wa Mkoa wa TABORA, AGGREY MWANRI kutoa wiki moja
Kamanda wa Polisi Mkoa wa TABORA, Kamshna Msaidizi HAMIS SELEMAN ISSAH
Polisi Mkoani TABORA imekamata Bunduki NNE zilizokuwa zinatoroshwa ikiwa ni siku kadhaa baada ya Mkuu wa Mkoa wa TABORA, AGGREY MWANRI kutoa wiki moja kwa wanaomiliki sihala kinyume cha sheria katika eneo la USINGE Wilayani KALIUA kuzisalimisha kwa hiari,.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa TABORA, Kamshna Msaidizi HAMIS SELEMAN ISSAH amesema silaha hizo zilikuwa zinatoroshwa kwenda maeneo mengine baada ya amri ya Mkuu wa Mkoa.
Kamanda HAMIS amesema watuhumiwa WANNE wamekamatiwa Wilaya ya SIKONGE na kuongeza kuwa huenda silaha hizo zilikuwa zinatoroshwa kutoka USINGE Wilayani KALIUA ambako silaha nyingi za kivita zinapatikana.
Kamanda HAMIS amewasihi wananchi wanaomiliki silaha kinyume cha sheria kuzisalimisha kwa hiari kwa kipindi walichopewa na baada ya hapo msako mkali utafanyika.

No comments