Serikali yapiga marufuku benki kukopesha kwa dhamana ya ofa ya viwanja
Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi WILLIAM LUKUVI amepiga marufuku
benki zote nchini kutoa mikopo kwa kutumia dhamana ya viwanja vyenye
ofa
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi WILLIAM
LUKUVI amepiga marufuku benki zote nchini kutoa mikopo kwa kutumia
dhamana ya viwanja vyenye ofa badala yake amewataka watumie viwanja
vyenye hati.
Waziri LUKUVI ametoa kauli hiyo jijini DAR ES SALAAM alipokutana na kufanya mazungumzo na jumuiya ya wenye mabenki nchini kujadili jinsi watakavyochangia kuongeza kasi ya watanzania kupimiwa viwanja na utatuzi wa changamoto mbalimbali zilizo kwenye sekta ya ukopeshaji kupitia ardhi.
Halikadhalika Waziri LUKUVI amezitaka benki kuhakikisha zinakua na mfumo wa ufuatiliaji wateja wanaokopa fedha kwa ajili ya miradi ya kilimo ili kujiridhisha kama fedha hizo zimetumika kama zilivyoombwa ama vinginevyo.
Na Elisha Elia
15 April 2016

No comments