• Breaking News

    Sekta binafsi yashauriwa kupendekeza utekelezaji malengo ya milenia


    Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN ameiagiza sekta binafsi nchini kujadili na kutoa mapendekezo ya namna itakavyoshiriki kwenye utekelezaji wa malengo mapya ya maendeleo
    Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akifungua mkutano wa kwanza unaojadili kuhusu kuangalia Biashara na Sekta Binafsi katika kuleta Maendeleo endelevu Nchini kwa ajili ya kufikia malengo 17 ya Maendeleo kwa Jamii
     
    Makamu wa Rais SAMIA SULUHU HASSAN ameiagiza sekta binafsi nchini kujadili na kutoa mapendekezo ya namna itakavyoshiriki kwenye utekelezaji wa malengo mapya ya maendeleo ikiwa ni njia mpya na bora ya maendeleo kuliko malengo ya awali ya milenia ambayo yalitekelezwa na kusimamiwa kwa kiasi kikubwa na serikali.

    Makamu wa Rais amesema hayo jijini DAR ES SALAAM  baada ya kufungua mkutano wa kwanza kwa wafanyabiashara na wadau wa sekta binafsi unaokutana kuangalia watakavyoshirikiana na serikali kufanikisha malengo mapya 17 ya milenia.

    Awali katika uwasilishaji wa mada zao mbalimbali za utangulizi mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa - UNDP, ALVARO RODRIGUES pamoja na Afisa Mtendaji mkuu wa taasisi ya biashara ya Afrika RAYMOND MUBAYIWA wamesema wanaamini ushirikiano huo utaiwezesha Tanzania kupiga hatua kiuchumi.

    Na Elisha Elia
    15 April 2016

    No comments

    Post Top Ad